Head of Primary Medical
Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni mratibu wa mradi wa
Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo
Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya
Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama
Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan
Hospital Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw.
Amin Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis
Nazrani.
Mkurugenzi Mkuu na
Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege (wa pili
kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa kwa hospitali
ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa
sasa vinawahusisha akinamama na watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za
awali za haraka zikiwemo usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari
hayo.
Aidha amesema Ndege Medics
inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa kujaribu kuokoa maisha ya akina mama
na watoto ambao lengo lake ni kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama
na watoto wachanga katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na
Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti
wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria
kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika
mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto
Tanzania
Mmoja wa wafanyakazi wa
Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya
kisasa.
Pichani Juu na Chini ni
muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali
ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama
Mjamzito na Mtoto Tanzania.
Pichani Juu na chini ni
baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Medics, Hospitali ya Aga Khan na
waandishi wa habari walioshuhudia tukio la makabidhiano
hayo.
Baadhi ya magari ya kubebea
wagonjwa yaliyokabidhiwa rasmi leo kwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar ikiwa ni
sehemu ya mradi Endelevu utakaohusisha Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na
Morogoro kwa ajili ya kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na
Mtoto.
Post a Comment