Demba Ba akishikilia jezi ya Chelsea wakati akitambulishwa kujiunga nayo |
Demba Ba (kulia) akishikilia jezi ya klabu yake mpya ya Chelsea pamoja na kocha Rafa Benitez |
CHELSEA imemsajili straika Demba Ba kutoka
Newcastle kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa ada ya uhamisho ambayo
haitajwi.
Inaaminikwa kwamba mkataba wa Ba na Newcastle
ulikuwa na kipengele kinachomruhusu kuzungumza na klabu nyingine ikija ofa ya
paundi milioni 7.
"Ni raha kuwapo hapa, nina furaha sana na
najivunia," straika huyo mwenye umri wa miaka 27 aliiambia tovuti ya klabu ya
Chelsea.
"Ilikuwa ni muhimu kwangu, na kwa Newcastle,
kumaliza suala la hatma yangu na sasa tunaweza kusonga mbele."
Straika huyo wa Senegal aliongeza: "Hivi sasa
wana mwezi mzima wa kusajili mchezaji mwingine. Mimi niko hapa sasa na nahitaji
kupazoea.
"Pale klabu iliyoshinda ubingwa wa LIgi ya
Klabu Bingwa Ulaya inapokuhitaji, inakuwa ni rahisi sana kufanya maamuzi. Hii ni
klabu kubwa na hilo limesaidia katika kufanya maamuzi. Hayakuwa maamuzi
magumu."
Ba, ambaye alihamia Newcastle akitokea West
Ham Juni 2011, amechukua nafasi ya Daniel Sturridge, ambaye ameondoka Stamford
Bridge kwenda kujiunga na Liverpool wiki hii.
Straika huyo mpya atakuwa tayari kucheza
mechi ya Kombe la FA kesho dhidi ya Southampton na nusu fainali ya Kombe la Ligi
dhidi ya Swansea, lakini hataweza kuichezea Chelsea katika Ligi ya Europa, kwani
tayari amecheza michuano hiyo akiwa na Newcastle.
Ba amefunga magoli 13 akiwa na Newcastle
msimu huu. Kutua kwake kutasaidia kumpunguzia mzigo straika aliyesajiliwa kwa
paundi milioni 50, Fernando Torres.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 28
amefunga magoli 14 msimu huu, ingawa ni saba tu aliyofunga kwenye ligi.
Post a Comment