Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), (kushoto) akisalimiana na
Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa Madagascar mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Januari,
2013. Mhe. Rais Rajoelina yupo nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano
unaoendelea wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi
za Kusini mwa Afrika
(SADC-TROIKA).
|
Mhe. Rais Rajoelina
akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya
kuwasili.
|
Mhe. Rais Rajoelina akiwa
amefuatana na Mhe. Membe mara baada ya
kupokelewa.
|
Mhe. Rais Rajoelina akipita
katikati ya Gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake huku akisindikizwa na Mhe.
Membe
|
Mhe. Rais Rajoelina akiwa
na Mhe. Membe wakifurahia burudani ya ngoma za utamaduni zilizokuwepo Uwanjani
hapo mara baada ya kuwasili
|
Post a Comment