Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es
Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa
Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564
zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi
Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri
Salama na Usalama wetu kwanza.
Makabidhiano hayo
yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na
kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi
hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es
Salaam, Naibu Kamishina wa Polisi Suleiman Kova akijaribhu mkuwasha moja ya
pikipiki zilizotolewa kwa maofisa mbalimbali wa jeshi hilo nch nzima mara baada
ya makabidhiano anayeangalia katikati na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said
Mwema na kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw.
Sabasaba
Afande Inspekta Mkweru
akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo kwa maafisa wa jeshi
hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu
ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa
Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu
ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova
Maafisa mbalimbali wa jeshi
la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Maafisa mbalimbali wa jeshi
la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Kamishna wa Operesheni wa
Jeshi la Polisi Paul Chagonjaakizungumza jambo na Msemaji wa Jeshi la Polisi
nchini Tanzania Advera Senso wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya pikipiki
zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi leo
Post a Comment