Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SEFUE: RAIS ASIPUNGUZIWE MADARAKA!!

KAZI ya utoaji maoni kwa ajili ya Katiba mpya imeendelea kwa kasi, huku Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akimkingia kifua rais ajaye kuwa kama atanyang’anywa madaraka yaliyopo kwenye Katiba ya sasa, atashindwa kuongoza nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, baada ya kuwasilisha maoni yake kwenye Tume ya Kukusanya maoni, Sefue alisema nafasi ya Rais inapaswa kuwa imara na yenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania wote.

“Asilimia kubwa ya Watanzania, wamekuwa wakipendekeza rais apunguziwe madaraka aliyonayo, jambo ambalo linaweza kuleta hatari mbeleni, suala hili linatupasa kuwa makini.

“Unajua unaweza kupunguza madaraka ya Rais kiasi ambacho kitamfanya ashindwe kutuunganisha na kuliongoza taifa kwa sababu tayari umedhoofisha nafasi yake.

“Tusiwe wepesi wa kutamka maneno bila ya kutafakari hasara na faida zake, tunapaswa kutambua taifa letu lenye miaka 51 ya uhuru bado masikini, kuna mataifa yenye miaka 200 hadi 400, lakini kamwe hayathubutu kumpunguzia Rais madaraka,” alisema.


Source: Mtanzania 16/01/13
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top