SERIKALI imekata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga uliomuondoa madarakani aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly (CCM).
Rufaa hiyo imewasilishwa Januari 10 mwaka huu katika Mahakama ya Rufaa chini ya hati ya dharura kwa kuwa jimbo hilo halina mwakilishi tangu Aprili 30 mwaka jana tangu Jaji Bathuel Mmila wa Mahakama hiyo alipofuta matokeo ya uchaguzi huo.
Imedaiwa kuwa ama rufaa hiyo haitasikilizwa na kutolewa uamuzi mapema, wakazi wa Sumbawanga mjini wataendelea kukaa bila kuwa na mwakilishi.
Warufani katika rufaa hiyo, ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kitandala Justus Kasilau na Vistus Kafupi, huku wajibu rufani wakiwa ni aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA, Noberty Yamsebo na Hilaly.
Warufani hao wameiomba mahakama kutoa amri ya kufuta hukumu hiyo, kuweka pembeni kikazia hukumu pia itangaze kuwa uchaguzi wa jimbo hilo ulikuwa huru na wa haki na matokeo yalikuwa halali. Katika rufaa hiyo, Mwanasheria Mkuu ametoa sababu 10 zinazoelezea makosa yaliyofanywa na Mahakama.
Source: Habari Leo
Alfajiri
2 hours ago
Post a Comment