Shelukindo. 
Mbunge wa Monduli
(CCM), Edward Lowassa
MBUNGE wa Kilindi (CCM),
Beatrice Shelukindo ametangaza kuchukua kile alichokiita uamuzi mgumu ili
kuhakikisha kuwa Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa anamrithi Rais Jakaya
Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Shelukindo alitoa kauli
hiyo Jumapili wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa
kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT katika sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya
zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa ambazo pia zilihudhuriwa na makada kadhaa wa
CCM.
Jana alipoulizwa kuhusu
kauli hiyo, Shelukindo alisema.
“Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa, ila pale (mkutanoni) sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato wa kumpata Rais haujafika.”
“Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa, ila pale (mkutanoni) sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato wa kumpata Rais haujafika.”
“Niliposimama
niliwaeleza kuwa nisingeweza kuchangia fedha nyingi kwa sababu watu wangu wana
njaa huko Kilindi. Pia kule (Kilindi) tunaendesha harambee ya aina
hiyohiyo.
Ila nikawaambia zawadi yangu kwa Wanamonduli ni kufanya uamuzi mgumu ili mwaka 2015 apatikane Rais mzalendo na anayeweza kufanya uamuzi mgumu na kwa wakati.”
Ila nikawaambia zawadi yangu kwa Wanamonduli ni kufanya uamuzi mgumu ili mwaka 2015 apatikane Rais mzalendo na anayeweza kufanya uamuzi mgumu na kwa wakati.”
Shelukindo aliendelea:
“Niliposema hivyo, umati uliibuka kwa shangwe na kunitaka nimtaje
nitakayeshirikiana naye, lakini nikawaambia kuwa huu si wakati mwafaka ila
baadaye nilichangia Sh500,000.”
Shelukindo alisema
harambee hiyo ilitarajiwa kuchangishwa Sh100 milioni lakini zikapatikana Sh70
milioni.
Mbali na Shelukindo,
makada wengine wa CCM waliohudhuria sherehe hizo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki,
Andrew Chenge, Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba na Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Shinyanga, Hamis Mngeja.
Awali, akizungumza
katika sherehe hizo, Lowassa aliwataka Watanzania kutumia mwaka huu wa 2013
kufanya uamuzi mgumu katika kila changamoto inayowakabili.
“Salamu zangu za Mwaka
Mpya kwa Watanzania:
Nawaomba wapitishe uamuzi mgumu kwa kila changamoto watakazokabiliana nazo,” alisema. Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na umaskini na kuongeza kuwa mtu akiamua inawezekana.
Nawaomba wapitishe uamuzi mgumu kwa kila changamoto watakazokabiliana nazo,” alisema. Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na umaskini na kuongeza kuwa mtu akiamua inawezekana.
Lowassa aliwahi kusema
bungeni akiitaka Serikali kuwa na tabia ya kupitisha ‘uamuzi mgumu’ katika
kuwaondolea wananchi kero akisema bila kuthubutu ni vigumu kukabiliana na
changamoto.
Katika sherehe hizo,
Lowassa pia alizungumzia taarifa zilizozagaa mitandaoni kuwa sherehe yake hiyo
ilikuwa ni ya kisiasa akisema:
“Wameandika katika mitandao ya kijamii kuwa kuna sherehe kubwa ya kisiasa.
Mimi nawaambia wa waache porojo hizo.
Nimekuwa nikiandaa sherehe hizi tangu mwaka 1995, wao wakitaka waige mfano huu.”
“Wameandika katika mitandao ya kijamii kuwa kuna sherehe kubwa ya kisiasa.
Mimi nawaambia wa waache porojo hizo.
Nimekuwa nikiandaa sherehe hizi tangu mwaka 1995, wao wakitaka waige mfano huu.”
Post a Comment