
MCHAKATO WA MISS UTALII
TANZANIA NGAZI ZA MIKOA WAKAMILIKA
KAMBI RASMI YA FAINALI ZA
TAIFA KUANZA JUMAMOSI WIKI IJAYO
Fainali za mashindano ya
Miss Utalii Tanzania na mchakato wa kuwapata wawakilishi wa mikoa katika Fainali
za Taifa za Miss Utalii Tanzania umekamilika katika mikoa yote ya
Tanzania.
Mikoa hiyo na majina ya
warembo katika mabano ni Arusha(Rose Godwin),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas), Dar
es Salaam 1(Sophia Yusuph 21) ,Dar es Salaam 2(Ivon Stephen,21) ,Dodoma(Erica
Elibariki,20), Geita (Jamia Abdul,19), Iringa(Debora Jacob Mwansepeta ), Kagera
(), Kilimanjaro(Anna Pogaly,23), Kigoma ( Zena Sultan,18), Katavi (Asha
Ramadhani,22), Lindi (Joan John,18), Mara(Doreen Bukoli,18), Mbeya (Dayana
Joachim,19), Mwanza(Jessica Peter Rugalabamu,18), Mtwara (Halima Hamis
Suleman,19), Morogoro ( Hadija Saidi,21), Manyara (Mary Chrysostom Rutta,18)
Njombe (Paulina Renard Mgeni,20), Pwani (), Rukwa (Anganile Rogers Emmanuel
,22), Ruvuma( Furaha Amon Kinyunyu ,23), Singida (Neema Julius,20), Simiyu
(Flora Msangi,22), Shinyanga (Lightness Kitua,19),Tabora (Magreth Michael
Malale,20 ),Tanga (Sarafina Jackson Chales,18),Vyuo Vukuu 1(Irine Richard
Makoye,21), Vyuo Vikuu 2 (Hawa Nyange, 22)
Washindi wa kwanza na wa
pili wa kila mkoa watawakilisha mikoa yao, katika Fainali za Taifa za Miss
Utalii Tanzania mwaka huu,fainali ambazo zimepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi
huu,katika Ukumbi wa Dar Live Dar es Salaam. Fainali za mwaka huu zitatanguliwa
na kambi ya siku 21 ya washiriki wote itakayo kuwa katika Hoteli ya kitalii ya
Ikondelelo Lodge Dar es Salaam.
Maandalizi kwa ajili ya
kuanza rasmi kambi ya Taifa yanaendelea na yamekamilika kwa zaidi ya 96%,tupo
katika hatua za mwisho za kukamilisha Taratibu za Baraza La Sanaa la
Taifa,ukiwemo kulipa ada ya shindano ya shilingi 1,500,00.00,kabla ya uzinduzi
rasmi wa kambi utakao fanyika katika hoteli ya Ikondelelo, Kibamba Dar es
Salaam,tarehe 8-1-2013.
Washiriki wote watawania
taji la Miss Utalii Tanzania 2012/13 .sambamba na tuzo 28 mbalimbali za heshima
za Jamii, Elimu ya Jamii, Afya ya Jamii,Utalii, Utamaduni, Uchumi, Miundo Mbinu
ya Utalii, Uwekezaji ,Madini na Maliasili mbalimbali za
Taifa.
Fainali za Taifa za mwaka
huu ,zitakuwa ni za Tano tangu kusajiliwa rasmi na serikali na mamlaka za haki
miliki za kutaifa na kimataifa mwaka 2002,katika kipindi hicho tumefanikiwa
kutwaa mataji katika kila mashindano ya Dunia na kimataifa tuliyoshiriki,ambapo
hadi sasa tunashikilia zaidi ya mataji matano ya Dunia na kumataifa. Mataji hayo
ni pamoja na Miss Tourism World 2005- Africa, Miss Tourism world 2006-SADC, Miss
Tourism World 2007-Africa,Model Of The World 2006-Personality, Miss Africa
2006-1STRunner Up na Miss Tourism World
2008-Internet.
Asante,
Erasto Gideon
Chipungahelo
Post a Comment