Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Shein
Na
Maelezo Zanzibar
Sherehe
za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaanza rasmi kesho kwa kazi za kufanya
usafi wa mazingira katika Wilaya zote za Unguja na
Pemba.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya kitaifa imeonesha kuwa Miradi ipatayo 62 inatarajiwa kuzinduliwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya kitaifa imeonesha kuwa Miradi ipatayo 62 inatarajiwa kuzinduliwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atafungua Skuli mpya ya
Sekondari ya Mlimani, iliyopo Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni Shamra
shamra za Sherehe hizo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein naye
atazindua miradi mbalimbali ikiwemo Ufunguzi wa Jengo la Chuo cha Utawala wa
Umma huko Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Pia
atafungua mradi wa E-Government katika Wilaya ya Magharibi Unguja na kufungua
Skuli mpya ya Sekondari ya Umoja, iliyopo Uzini Wilaya ya Kati Unguja pamoja na
kuzindua Barabara kutoka Mfenesini hadi Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B
Unguja.
Hali
kadhalika Dkt.Shein atafungua Mradi wa kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia
kwenda Dijitali na Ufunguzi wa Studio ya kurikodia Sanaa na Muziki ambapo kwa
upande wa Pemba atafungua Skuli mpya ya Sekondari ya Shamiani iliyopo
Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Mbali
na Shughuli hizo siku ya kilele hapo January 12 kwenye Uwanja wa Amani Rais
Shein atakagua Gwaride lililoandaliwa na Vikosi vya ulinzi na usalama na Vikosi
vya SMZ pamoja na kulihutubia Taifa na Usiku kuhudhuria Taarab rasmi huko katika
Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani
Naye
Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad atafanya uzinduzi mbali mbali
kwa ufunguzi wa Skuli na Maabara wakati Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd
atafanya Shughuli kama hizo kwa ufunguzi wa Skuli na Majengo mapya ya nyumba za
Wazee zilizopo Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.
Mbali
na shughuli hizo baadhi ya Marais wastaafu,Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Muungano watafanya shughuli za ufunguzi wa Miradi mingine
ikiwemo ya Maji, Skuli na Mradi wa Mnara wa Radio wa Masafa ya Kati uliopo Bungi
Wilaya ya Kati Unguja.
Post a Comment