Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA


6029AFC0-AFF0-4C91-B402-D2E48ADB0A9A_w640_r1_s
SHIRIKA  la Jhpiego  la jijini Dar es saalam limefanikiwa kubuni aina mpya ya mradi ujulikao kama Maisha ambapo mradi huo utaweza kutumia simu za mkononi kwa ajili ya kufuatilia afya za mama wajawazito  kwa malengo ya kupunguza vifo vya wajawazito
  Meneja mradi wa shirika hilo Dkt Dunstan Bishanga alisema kuwa mradi huo wa maisha umeanza kutekelezwa kwa mkoa wa Morogoro
 Dkt Bishanga aliongeza kuwa mradi huo una malengo ya kuhakikisha kuwa inapunguza vifo vya mama wajawazito hapa nnchini lakini njia pekee ya kuwakutanisha wahudumu wa afya pamoja na wajawazito ni simu za mkononi hasa  kwa kuwapa wajawazito taarifa mbalimbali
 Pia alisema kuwa Mradi huo ambao kwa sasa umeanza kutumika katika Mkoa wa Morogoro lakini wanaendelea kufanya tathimini mbalimbali za kuhakikisha kuwa unasambaa nchi nzima kwani una uwezo mkubwa sana wa kuokoa maisha ya mama wajawazito

 Hataivyo aliongeza kuwa mara baada ya mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi huo wataweza kwenda mikoani ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu zaidi ili kuimarisha zaidi afya ya mama kwa manufaa ya Nchi nzima kwani vifo hivyo vinasababisha sana Umaskini katika jamii.
 Awali alisema kuwa suala la mama wajawazito ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa tahadhari kubwa sana ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu sahihi za afya kutoka kwa wataalamu hivyo nao wazazi wa kiume wana nafasi kubwa sana ya kufanya hivyo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top