Sentahafu
wa Zambia Stopilla Sunzu amechukua likizo fupi kutoka kwenye kambi ya timu
ya taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2013 ili apate nafasi ya kwenda nchini
England kwenda kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu
hiyo.
Sunzu ambaye anachezea klabu ya TP Mazembe ya
DRC ambayo imeandika kwenye mtandao wake kwamba ada ya uhamisho ya $4.8million
imeshakubaliwa na kilichobakia ni mchezaji kukamilisha vipimo vya
afya.
Mfungaji huyo wa penati ya ushindi ya Zambia
dhidi ya Ivory Coast katika AFCON 2012, anatarajia kurudi Afrika ya kusini
January 19, siku mbili kabla ya mabingwa watetezi kuchuana na Ethiopia katika
mechi ya ufunguzi.
Post a Comment