DAR ES SALAAM,
Tanzania
MAALIM Hassan Yahya Hussein,
amepinga kauli iliyotolewa hivi karibuni na mtabiri mwenzake kuwa rais wa mwaka
2015 kuwa atakuwa mwanamke.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu utabiri wake wa matukio yatakayotokea
mwaka 2013, ambapo mwaka huo utaanza Machi 21 mwaka
huu.
Maalim Hussein alisema
kiutabiri huwezi kutoa utabiri katika matukio ya mwaka mmoja mbele, kitendo cha
mtabiri huyo ni sawa na kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wenye nia ya kutaka
kugombea nafasi hiyo mwaka 2015.
“Huwezi kutoa utabiri wa
miaka miwili mbele hata Sheikh Yahya Hussein mtabiri aliyekuwa akikubalika
hakuwahi kufanya hivyo, pia sikubaliani naye kuwa rais ajaye atakuwa mwanamke
hata ukiangalia katika njia zetu za utabiri ambazo ni namba zinapingana na
hilo”alisema.
Alisema matokeo ya utabiri
kama huo ni sawa na uwamuzi wa kuwafungia milango kidemokrasia baadhi ya
wanasiasa wenye nia ya kugombea urais mwaka 2015.
“Kuna baadhi ya viongozi
wakiwemo Lowassa na Membe wanadaiwa kuwa huenda wakagombea nafasi hiyo, kwa
kufanya hivyo itakuwa ni kuwakatisha tamaa”alisema.
Akizungumzia utabiri wa mwaka
huu, alisema kuwa kuna viongozi wengi, wabunge, wakuu wa mikoa na wengine
watatoa matamshi ya utatanishi na kusababisha hofu na mitafaruku itakayowafanya
watu kupigana.
Vile vile alisema wapo
wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wataungana katika
masuala ya msingi yatakayohusu utaifa bila kujali itikadi zao za kivyama au
kimajimbo.
Maalim Hussein alibainisha
kuwa Rais Jakaya Kikwete ataunganisha nchi na kuwa moja yenye uimara wa utaifa
kuliko watangulizi wake, akishirikiana zaidi na wanasiasa na viongozi wa dini
kuondoa mtikisiko wa uvunjifu wa amani uliyojitokea mwaka
jana.
Aidha, Chama kimoja cha siasa
kitajitokeza na kitachochea kujitenga na kuunda Taifa lake hata hivyo, kusudio
hilo halitafanikiwa kwani litapingwa na Watanzania wote kwa kauli moja na
vitendo.
Maalim Hussein pia alisema
kutatokea vifo vya ghafla kwa watunzi wa hadithi na vitabu, wandishi wa habari,
wanasiasa na wasanii ambapo matukio hayo yatakuwa mabaya zaidi kuliko mwaka
jana.
Akigusia Uchaguzi Mkuu
utakaofanyika hivi karibuni nchini Kenya ambao ni majirani, alisema kuwa
Muungano wa CORD, ukiongozwa na Raila Odinga utashinda uchaguzi huo, ambao ana
amini utakuwa wa amani na tulivu.
“Ushindi huo utakuja baada ya
kuushinda Muungano wa Jubilee ukiongozwa na akina Uhuru Kenyata na Ruto pamoja
na ule wa Musalia Mudavadi unaoitwa AMANI”alisema.
Post a Comment