TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika-SADC (TROIKA) ataongoza kikao cha Wakuu wa Nchi tatu zinazounda Asasi
hiyo kinachotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Alhamisi tarehe 10 Januari,
2013.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitajadili maendeleo ya
hali ya siasa nchini Madagascar na hali ya usalama Mashariki ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Viongozi wanaotarajiwa
kuhudhuria kikao hicho ni Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia ambaye ni Makamu
Mwenyekiti wa Troika, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Armando Emilio
Guebuza wa Msumbiji.
Aidha, kikao hicho
kitatanguliwa na kikao cha Mawaziri kitakachofanyika katika Hoteli ya Hyatt
Regency (Kilimanjaro) ya jijini Dar es Salaam tarehe 09 Januari,
2013.
Nchi tatu za TROIKA ni
Afrika Kusini, Namibia na Tanzania, ambaye ndiye Mwenyekiti. Nchi ya Msumbiji
inashiriki kama Mwenyekiti wa sasa wa SADC.
IMETOLEWA
NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES
SALAAM.
08
JANUARI, 2013
Post a Comment