Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akikata Utepe
kuonyesha Ufunguzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia Matangazo ya Dijitall huko
Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za
Kutimia Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
SHIRIKA la Utangazaji
Zanzibar ZBC limetakiwa kuhakikisha kwamba linafanyakazi kwa ufanisi mkubwa
kulingana na mfumo uliopo hivi sasa.
Alisema kuwa wafanyakazi wa
shirika hilo wameonakana wakifanya kazi kimazowea tu bila kufuata taratibu za
kikazi.
Hayo yameelezwa leo na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein katika
Uzinduzi wa Miundombinu ya Dijitali na Jengo la Studio ya
Kisasa
Alisema kuwa kubadilika kwa
watendaji kazi ni suala la lazima kutokana na mabadiliko makubwa yalioko duniani
.
Dkt Shein alisema kuwa ZBC
wananchi wengi wanapiga kelele juu ya utendaji wa wafanyakazi wa ZBC kutokana
na vipindi vyao kutoridhisha na kukatika katika kwa matangazo yao zaidi wakati
wa taarifa ya habari.
Alisema kuwa Zanzibar
inaheshima yakekatika masuala ya Utangazaji kwani Redio nyingi za Nje
zinawatangazaji kutoka Zanzibar ambao ni mahiri katika masuala ya
Utangazaji.
Dkt Shein amesema kuwa hivi
sasa hatoweza kuvumilia tena kutokana na utendajihuo ambao hauridhishi hata
kidogo na hasa sasa tulivyoingia katika mfumo huu wa
DIGITALI.
“Sitaki kuiona Serikali
ambayo nnayoiongoza mie iwe ‘tiro’(mwisho) alisema Dkt
Shein.
Alisema kuwa kuingia katika
mfumo mpya wa dijitali ni kazi kubwa lazima watendaji wafanyekazi kwa
mashirikiano na kuwe na uwiano baina yao ili kuweze kuwa na kiwango ambacho
kitaweza kuwajengea sifa wafanyakazi hao.
Alieleza kuwa madhumuni
makubwa ya Mapinduzi ni kuweza kuwakomboa wanyonge na kuwabadilisha maisha yao
sitofurahishwa na kuona gharama zote zilizotumika katika kuingia katika mfumo
huo mpya wa Digitali kuweza kupotea bure lazima viongozi waweze kusimamia
majukumu yao na kuanzia hivi sasa lazima mambo yende.
‘’Hakuna aliekamilika
lakini tujitahidi’’ alisema Dkt Shein .
Dkt Shein alimtaka Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk pamoja na Katibu
wake kuisimamia ipasavyo Shirika hilo la ZBC na kuhakikishakuwa mambo yanakwenda
vizuri.
Akizungumzia juu ya Studio
ya Kurikodia Dkt Shein amesema kuwa madhumuni ya kutengeneza Studio hiyo ni
kwaajili ya Wasanii wa Zanzibar waweze kupata nafasi nzuri za kurekodia nyimbo
zao na hapo hapo kuwa na pahala ambapo wataweza kurekodi michezo ya kuigiza
napia kuonesha maigizo mbali mbali katika ukumbi huo.
Nae
Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema
kuwa miundombinu mipya ya Digitali ni mkataba baina ya Serikali ya
Zanzibar na Kampuni ya Ágape na imeagharimu jumla ya Shs billion 8 za Tanzania
na kuweza kujengea vituo 6 vya kurushia matangazo vikiwamo vya Kizimkazi, Nungwi
na Masingini. Kwa upande wa Pemba ni Konde,Mizimiumbi na
Mkanjuni.
Aidha alisema kuwa ifikapo
tarehe 28 /2/ 2013 analogi itazimwa na kuanza mfumo mpya wa dijitali na
kuwaeleza wananchi wasiwe na wasiwasi ya upataji wa vingamuzi ambavyo vitakuwa
vyakisasa na madhubuti.
Said alisemakuwa vingamuzi
hivyo vitapatikana kwa katika sehemu mbali mbali za Wilaya zote kumi za
Zanzibar na hakutakuwa na haja kwa watu kufuatia Mijini.
Alisema kuwa kila kingamuzi
kimoja kinatarajiwa kuuzwa si zaidi ya shs za Tanzania 50,000 na malipo ya
matangazo yatakuwa si zaidi ya shiling za Tanzania 8000 vikiwa na chanal
36-38.
Post a Comment