Timu ya Taifa (Taifa Stars)
itacheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Januari
11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Addis Ababa,
Ethiopia.
Stars chini ya Kocha Mkuu
Kim Poulsen inatarajia kuingia kambini jijini Dar es Salaam keshokutwa (Januari
6 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo. Mechi hiyo itakuwa kipimo cha mwisho kwa
Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Ethiopia iko kundi C
pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso. Ethiopia itacheza
mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Zambia.
Katika mechi yake ya
mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mechi hiyo ya kirafiki
dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco
kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa
Machi mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa
kambini ni Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi
Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir
Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani
(Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar
(Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank
Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa
Sugar).
Washambuliaji ni John
Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC),
Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wakati benchi la Ufundi
lina Kim, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa),
Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda
(Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
UCHAGUZI KWA WANACHAMA WA
TFF
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
inatarajia kukutana leo mchana (Januari 4 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo
mengine itapitia maendeleo ya uchaguzi kwa wanachama wa TFF ikiwemo Bodi ya Ligi
Kuu (TPL Board).
Wanachama wa TFF (vyama
vya mikoa) wote wameshafanya uchaguzi ukiondoa mikoa ya Rukwa na Katavi
inayotarajiwa kufanya uchaguzi baadaye mwezi huu. Kwa upande wa vyama shiriki
ambavyo bado havijafanya uchaguzi ni Makocha (TAFCA), Wachezaji (SPUTANZA),
Waamuzi (FRAT) na Tiba ya Michezo (TASMA).
Vilevile Kamati ya
Uchaguzi ya TFF baada ya kikao hicho huenda ikatangaza rasmi mchakato wa
uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka
huu.
Post a Comment