Wanachama wa Chama cha
United Democratic Forum (UDF) wamemteua rasmi Mwenyekiti wa Chama hicho na Naibu
Waziri Mkuu wa Kenya, Wycliffe Musalia Mudavadi kuwa mgombea rasmi wa Chama
hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Urais unaotaraji kufanyika Mwezi Machi mwaka
huu.
Mudavadi aliyezaliwa
Sabatia, wilayani Vihiga mwaka 1960 endapo atashinda Kinyang’anyiro hicho
anaweza kuwa Rais wa nne wa Jamhuri ya Watu wa Kenya na kabla ya kuhamia UDF
alikuwa ni Kiongozi wa Juu wa chama cha ODM kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa
Kenya, Raila Odinga.
Udavad alichaguliwa kwa
mara ya kwanza kuwa Mbunge wa jimbo la Sabnatia mwaka 1989 akitokea kambi ya
Upinzani Bungeni baada ya kuchukua nafasi ya BABA YAKE Mzee Moses
Mudavad.
Mwaka 2002 Mudavad alikuwa
ni Makamu wa Ras wa mwisho na ambaye alihudumu kwa kipoindi kifupi kuliko Makamu
wa Rais wote kipindi cha Utawala wa Rais Daniel Arap Moi, na alichaguliwa ili
ku;lifanya kabila la Luhya kuwa ndani ya chama cha KANU.
Mudavadi alikuwa ni Mgombea
mwenza wakati Uhuru Kenyatta akiwania Urais uchaguzi wa 2002.
Katika uchaguzi wa mwaka
2007, Mudavadi pia alikuwa Mgombea Mwenza wa Raila Odinga kupitia chama cha ODM,
ambacho kilizaliwa kutoka muungano wa Vyama vya ODM-K na kuangushwa na Rais wa
sasa wa Kenya, Mwai Kibaki na baade kukubaliana kuanzisha serijkali ya Mseto
ambapo Odinga aliteuliwa kuwa Wazziri Mkuu na Mudavadi kuteuliwa kuwa Naibu
waziri Mkuu kutoka ODM na Uhuru Kenyatta akiwa Naibu Waziri Mkuu kutoka PNU cha
Kibaki.
Baada ya kuanza kwa
harakati za Uchaguzi 2012, na kubadilika kwa Katiba ya Chama cha ODM yakuwa
Mwenyekiti wa Chama ndio akaamua kujiengua na kuumngana na Uhuru Kenyatta na
William Ruto na kuweka muungano wa vyama vya UDF, URP na TNA na baadae Mudavadi
akaondoka katika muungano huo baada ya kukiukwa moja ya kanuni za Muungano juu
ya mgombea Urais ambapo baadhi ya wafuasi wa Kenyatta walitaka ndie agombee
Urais kwa Umoja huo.
Post a Comment