WANAFUNZI wa chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wameilalamika bodi ya mikopo
nchini ucheleweshawaji wa fedha zao.
Malalamiko hayo yametolewa na baadhi wa wanafunzi wa chuo hicho wakidai kuwa umetokana na uzembe wa watumishi wa bodi, huku wakionesha hofu ya kuliwa kwa fedha hizo.
Walisema kuwa utendaji wa bodi ya mikopo unawafanya wanafunzi waishi maisha magumu kufikia hatua ya wengine kujiuza ili waweze kujikimu kimaisha.
“Ni muda mrefu umepita tangu tuahidiwe kwamba hizo pesa tutapewa lakini mpaka sasa hakuna kinachoeleweka ndiyo maana tuna mashaka na wahusika ndani ya bodi kwamba huenda fedha zetu zimetafunwa,”alisema mmoja wa wanafunzi kwa sharti la kutotajwa jina.
Aidha wanafunzi hao walishangazwa na ukimya wa bodi ya mikopo, hivyo hawaelewi hatma ya fedha zao kutokuingizwa kwa wakati hivyo huwalazimu kutafuta ahueni ya maisha kwa njia zisizopendeza.
Kadhalika wamedai kuwa wakati hali ikiwa hivyo, baadhi ya taarifa za wanafunzi kuhusiana na mikopo hazionekani, na wameambiwa wanatakiwa kujaza upya fomu kwa ajili ya kujisajili upya.
Msemaji wa bodi ya mikopo Veneranda Malima alisema suala hilo ni pana mno lakini alipotakiwa kutoa ufafanuzi, simu yake ilikatika na hata alipopigiwa tena haikuwa ikipokelewa.

Chanzo: Tanzania daima
Post a Comment