Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UFAFANUZI KUTOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI: GESI ASILIA YA LINDI NA MTWARA NI MALI YA TANZANIA


 


1.0 UTANGULIZI
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi wa miradi ya Gesi Asilia ambayo itatekelezwa kwa kushirikiana na wawekezaji katika Sekta
ndogo ya Gesi Asilia na kueleza manufaa makubwa yatakayopatikana
kwa wananchi wote wa Tanzania wakiwemo wale wa Mikoa ya Mtwara na
Lindi.
Siku ya Alhamisi, tarehe 27 Disemba 2012, baadhi ya Vyama vya Siasa
vya Upinzani viliratibu na kuhamasisha baadhi ya wakazi wa Mkoa wa
Mtwara, wengi wao wakitokea Mtwara Mjini kufanya maandamano ya
kudai raslimali ya Gesi Asilia iwanufaishe wakazi wa Mtwara na kupinga
mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara hadi
Dar es Salaam. Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa taarifa
ifuatayo kwa Wa-Tanzania wote kwa kupitia vyombo vya habari.
Tokea Uhuru, uchumi wa Tanzania umetegemea kilimo cha mazao ya
biashara kama vile katani (Tanga na Morogoro), pamba (Mwanza, Mara
na Shinyanga), kahawa (Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma na Mara), chai
(Iringa) na tumbaku (Tabora). Fedha za mazao haya zimewanufaisha
wakazi wa mikoa yote ya nchi yetu bila ubaguzi wo wote wala wakulima
wa kutoka mikoa hiyo hawajawahi kufanya maandamano wakidai
upendeleo (dhidi ya Wa-Tanzania wengine) wa aina yo yote ile.
1
Mapato yatokanayo na uchimbaji wa dhahabu (Mwanza, Geita, Mara,
Shinyanga na Tabora), almasi (Shinyanga) na tanzanite (Manyara)
yamewanufaisha Wa-Tanzania wote bila ubaguzi wo wote ule! Minofu ya
samaki wa Ziwa Victoria (Mara, Mwanza na Kagera) imeliingizia Taifa
letu fedha nyingi ambazo zimetumiwa na wakazi wa nchi nzima bila
ubaguzi wo wote.
Aidha kuna mikoa ambayo inazalisha mazao ya chakula kwa wingi kwa
manufaa ya Wa-Tanzania wote. Mahindi kutoka Rukwa, Mbeya, Ruvuma
na Iringa yanasafirishwa kwenda mikoa yote ya nchi yetu bila kujali eneo
yanakolimwa na wakazi wa mikoa hiyo hawajawahi kudai mahindi hayo
ni kwa ajili ya watu wa mikoa hiyo pekee. Sukari ya Kilombero, Mtibwa
na Kagera inatumiwa na wakazi wa mikoa yetu yote bila ya kuwepo
madai ya mikoa inayozalisha sukari hii kupewa upendeleo wa aina yo
yote ile. Maji ya Mto Ruvu yanatumiwa na wakazi wa Dar Es Salaam bila
manung’uniko yo yote kutoka kwa wakazi wa eneo la chanzo cha Mto
Ruvu.
Umeme wa kutoka Mtera, Kidatu na Kihansi (Dodoma na Morogoro),
Hale (Tanga), na Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro) unatumiwa na wakazi
wote wa Tanzania bila ubaguzi au malalamiko ya wenyeji wa sehemu
ambazo umeme huo unafuliwa na kusafirishwa kwenye Gridi ya Taifa.
Kwa hiyo, kutokana na mifano hii michache, ni wajibu wa wazalendo na
wapenda maendeleo wa kweli na hasa Wa-Tanzania wanaopinga ubaguzi
wa aina yo yote ile kujiuliza kwa kina sababu zilizopelekea Vyama Siasa
vya Upinzani kupanga, kuhamasisha, kushabikia na kuongoza
maandamano ya tarehe 27 Disemba 2012 pale Mtwara Mjini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top