Hawa ni waigizaji katika tasnia ya maigizo na filamu
hapa nchini.Walikutana katika filamu ya mboni yangu na kuwa wapenzi.Katika
mapenzi yao walivalishana pete za uchumba na hatimae kupanga kufunga ndoa.Siku
chache kabla ya ndoa yao walipata ajali na Wastara kuvunjika kabisa
mguu.
Watu wakajiuliza kweli Sajuki atamuoa Wastara pamoja na
kukatwa kabisa mguu?Baada ya wastara kupona jeraha ndoa yao ikafungwa dada
akitembea kwa magongo.Baadae alifanikiwa kupata mguu wa bandia na sasa
anatembelea mguu wa bandia.
Mitihani haikuishia hapo katika familia hii ambayo
wamejaaliwa mtoto
Baada ya
kurudi nchini hali yake ilikuwa nzuri tu na mwili ukaanza kurejea kama
anavyoonekana kwenye picha hapo akiwa na Wastara mkewe.Pamoja na kuwa
katika hali hii bado alikuwa ni mgojwa.
Mwezi wa kumi
na moja 2012 Sajuki alifanya tour aliyoiita asante Tanzania kwa lengo la
kuwashukuru watanzania walipomchangia.Lakini kilichokuwa nyuma ya pazia ni
kwamba alikuwa akikusanya pesa ili arudi India kwa matibabu.Akiwa mkoani
Arusha
katika Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid jijini hivi karibuni alianguka.Na yeye mwenyewe kukiri kwa kusema
“Sijisikii vizuri, hali yangu ni
mbaya.”
Baadae mwenyewe alisema
kuwa pamoja na kuumwa,haikuwa rahisi kurudi katika vyombo vya habari tena kwa ajili ya
kuomba Watanzania kumchangia kwa ajili ya fedha za matibabu kwa awamu nyingine.
na muda wa kurudi ulikuwa
umefika.
Kwa takribani
wiki mbili Sajuki alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake
kuzidi kuwa mbaya.Na ilifikia hatua ya mheshimiwa raisi Jakaya Mrisho Kikwete
kuamua kumsaidia kumpeleka India kwa matibabu.
Post a Comment