Michael Wambura, akisisitiza
jambo.
KATIBU
Mkuu wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa miguu (FAT), sasa Shirikisho la
Soka nchini (TFF), Michael Wambura, leo amechukua fomu za kuwania nafasi ya
Makamu wa Rais, katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka
huu.
Wambura
alichukua fomu jana za kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za TFF, ambapo pia
aliwaambia waandishi wa habari kuwa lengo lake ni kuchangia maendeleo ya mpira
wa miguu, baada ya kipindi cha Leodgar Tenga kumalizika.
Wambura
ameingia kwenye uchaguzi huo, huku akiwa na kumbukumbu ya kufanyiwa mizengwe,
ambapo hata hivyo mwenyewe alikiri kukubali yaliyofanywa na Rais anayemaliza
muda wake, Leodgar Tenga.
Akizungumza,
Wambura alisema,“Nimeamua kuchukua fomu kwa ajili ya kusaidiana na wadau wengine
wa michezo kukuza na kuendeleza mazuri yaliyofanywa katika kipindi cha Tenga,
ambaye hapana shaka ametangazaa kuwa hataendelea kugombea,”
alisema.
Ofisa
Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa mbali na Wambura, wengine sita
wamechukua fomu za kuwania ujumbe hivyo, hivyo kufikisha watu 27 waliochukua
fomu hizo.
Post a Comment