Azam na Kombe la Mapinduzi |
Na Mahmoud
Zubeiry
BAADA ya
kutwaa Kombe la Mapinduzi mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar, Azam FC
inatarajiwa kuondoka nchini Alhamisi kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya wiki
moja ya michezo ya kirafiki, kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Kombe
la Shirikisho.
Katibu Mkuu
wa Azam FC, Nassor Idrisa amesema leo kwamba katika
ziara hiyo watacheza mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya timu za Sofapaka, AFC
Leopards na Gor Mahia kabla ya kurejea nchini Januari
23.
Nassor
alisema ziara hiyo ni maalum kwa ajili ya kuiweka sawa timu yao kabla ya kuanza
kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na Kombe la Shirikisho
Afrika.
Nassor
amesema anaamini timu za Kenya ni nzuri na zitawapa changamoto nzuri kabla ya
kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na kuingia kwenye Kombe la
Shirikisho.
“Tumekuwa
katika programu ndefu ya maandalizi tangu Desemba, tukianzia Kongo (DRC) ambako
tulicheza mashindano na kuchukua Kombe, tumetoka tumeingia kwenye Kombe la
Mapinduzi tumeshiriki na kuchukua Kombe, na sasa tunakwenda Kenya,”alisema
Nassor.
Katibu huyo
alisema kikosi kizima cha Azam kitakwenda Kenya kwenye ziara hiyo na baada ya
hapo timu itarejea tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Post a Comment