Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za wilaya hiyo zilizopo Buswelu ilemela jijini Mwanza. |
Hilo limebainishwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya wilaya yake kwa msimu wa 2005 hadi 2012 mbele ya waandishi wa habari.
Baada ya kuwepo kwa uhaba huo wa vyumba vya madarasa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela imeanza mikakati ya ujenzi wa vyumba hivyo 24 vya madarasa unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu kwa lengo la kuweza kuchukuwa wanafunzi wote walioshindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari katika kata tisa za Halmashauri hiyo.
Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Uchumi wa wilaya Llemela Bw. Philip Nyakutonya amesema kuwa Jumla ya shilingi bilioni 3.2 zimetengwa katika ujenzi wa vyumba hivyo 24 vya madarasa
Post a Comment