Takriban watu 150 ikiwa ni pamoja na watoto, wamejeruhiwa leo wakati treni zilipogongana karibu na mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria.
Ajali hiyo imetokea wakati treni ilipojigonga katika treni nyingine iliyokuwa imesimama karibu na Attridgeville, ambacho ni kitongoji cha mji wa Pretoria.
Watu 20 wako katika hali mbaya , pamoja na kuwa wengi wameondoka katika eneo hilo huku wakiwa na majeraha.
Huduma za treni zimesitishwa kwa muda kutokana na ajali hiyo, ambapo sababu za ajali hiyo bado zinachunguzwa.
Post a Comment