Kamati
ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF
Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013,
ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na
kutoa maamuzi kama ifuatavyo:
1. Waombaji
uongozi wa TPL Board
(a) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi
ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili
pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said
Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumwondoa mwombaji uongozi
kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:
(i) Si Mwenyekiti wa Klabu ya
Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii) Si mkweli katika maelezo
aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa
pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za
Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote
kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa
pingamizi hiyo.
(b) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi
zilizowasilishwa na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma walioomba
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba,
kwamba Ndg. Yusufali Manji :
(i) Hana uzoefu wa uendeshaji
wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa
mpira wa miguu.
(ii) Hana sifa ya kuwa ama
mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira
wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(iii) Hana elimu ya kidato cha
nne
(iv) Ameshindwa kusimamia katiba ya
Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi
zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally
Magoma hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa
hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.
Kamati ya Uchaguzi ya TFFimezitupa pingamizi hizo.
(c) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba
kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili
pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi
ya Ndg. Hamad Yahya Juma,kwamba Ndg. Hamad Yahya Juma:
(i) Si Mwenyekiti wa Klabu ya
Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii) Si mkweli na mwadilifu na
amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa
kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa ya Kanuni za
Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote
kuthibitisha maelezo ya pingamizi.
2. Waombaji
uongozi wa TFF
(a) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi
aliwekewa pingamizi kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda
uliopangwa.
Kamati imeitupa
pingamizi ya Ndg. Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi
hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi
wake kuhusu pingamizi.
(b) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella
aliwekewa pingamizi na Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter
Naminga, kwamba Ndg. Mvella:
(i) Akiwa mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta maendeleo ya soka katika
ukanda huo.
(j) Ana kesi ya rushwa katika
mahakama ya wilaya ya Iringa
Kamati imeitupa
pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF
Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo
ya pingamizi.
(c) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati
ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie
Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:
(i) Alifanya ubadhilifu wa
fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza
(MZFA).
(ii) Alitumia madaraka yake
vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.
(iii) Alivunja Katiba ya MZFA na
FIFA
(iv) Anavuruga shughuli za
uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa wawekaji
pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na vielelezo
vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele
yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya hila na udanganyifu (collusion)
dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF
Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya
TFF imezitupa pingamizi hizo.
(d) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha
Galibona wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
kupitia Kanda ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa
pingamizi na Ndg. Paul Mhangwa kwamba hawana uzoefu wa uendeshaji wa
Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).
Kamati imeitupa
pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara
ya 11(2).
(e) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya
Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg.
Josea Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:
(i) Alikiuka Katiba ya TFF kwa
kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu masuala ya
uchaguzi.
(ii) Alikosa uadilifu kwa kutumia
kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi aliyokuwa aniongoza akiwa
Katibu Mkuu wa FAT.
(iii) Amekuwa akijaribu kupotosha
umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa kutumia haki na kuviita
‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).
(iv) Mwaka 2004 alikiri kwamba
alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa kuwa alikuwa akivipa pesa na
kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa sababu aliacha kuwapa waandishi
pesa.
(v) Mwaka 2004 alikataa
kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu wa FAT iwe ya
kuajiliwa.
(vi) Alikosa uwezo wa kutekeleza
wajibu na malengo ya TFF.
Ndg.
Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg.
Wambura. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa
kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya
11(2).
(f) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF;
Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:
(i) Alivunja Katiba ya TFF kwa
kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama wa TFF kikiwemo Chama chake
cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na
FIFA baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya
Katiba kwa njia ya Waraka, ambayo yalihusisha pia maagizo ya FIFA na
CAF
(ii) Hana sifa ya uzoefu wa miaka
mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
(iii) Anakosa uadilifu na haiba ya
kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.
Kamati imeitupa
pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea
wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu
pingamizi hilo.
(g) Pingamizi
dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa
TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg.
Medard Justiniani kwamba:
(i) Ni Hakimu Mkazi katika
Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi wa umma hivyo alikosa kigezo
na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.
(ii) Anakatazwa na Judicial
Service Act, Public Service Act 2002 na Code of Conduct for
Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya Rais wa
TFF.
(iii) Kutakuwa na Mgoganao wa
kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais wa TFF.
(iv) Amekosa umakini na uadilifu
kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na
TRA.
Ndg.
Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa na
Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa kuwa
alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi
lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa pingamizi
hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.
Angetile
Osiah
KATIBU
KAMATI YA
UCHAGUZI

Post a Comment