Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega, (kushoto) akishuhudia zoezi la utiaji wa sahihi wa mkataba huo wa miaka mitatu kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Addo Mapunda akitiliana saini na Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo Bi Anne Devilliers, wakati wa hafla hiyo fupi ya kutiliana saini iliyofanyika leo. |
Makabidhiano.
Na Abdulaziz Video,Lindi
JUMLA ya wanafunzi wapatao
1,580 wanaosoma Shule tisa za Sekondari,wilayani Kilwa, mkoani
Lindi,watanufaika na mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya
teknolojia ya kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African
Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na
uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.
Mradi
huo wa miaka mitatu,utagharimu jumla ya Sh, 144,945,218/-zitakazotumika kujenga
misingi bora ya Lugha ya kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia
mwaka 2013. Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya
hiyo, Adoh Mapunda,alipokuwa akitoa taarifa katika hafla fupi ya
kutiliana
na
saini ya utekelezaji wa mpango huo.
Mapunda
alisema mpango huo,utakaochukuwa takribani muda wa kipindi cha miaka
mitatu,umeanza rasmi mwezi huu kwa wanafunzi wapatao 1,580 wa kidato cha kwanza
kutoka Shule tisa za Sekondari zilizopo katika
Amezitaja Sekondari zitakazonufaika na
mpango huo kuwa ni,Kilwa day iliyopo mji mdogo wa masoko, Mtanga, Songosongo,
Mbuyuni, Kinjumbi,Miteja,Mingumbi,Kikanda na Sekondari ya wasichana ya
Ilulu.
Mkurugenzi Mapunda alisema mafunzo hayo
kwa kuanzia yatakuwa ni ya wiki sita,yameanza rasmi hivi karibuni na kwamba
walimu wapatao 30 wakiwemo (12) wa kigeni (Volunteers) wakiwemo na walimu wazawa
(18).
“Hizi
Shule tisa kila moja italazimika kutoa walimu wawili watakaopatiwa mafunzo kwa
ajili ya kuendesha mpango huu katika Shule zote hizo”Alisema
Mapunda.
Aidha,
Mapunda alisema kupitia ufadhili wa mpango huo wa mafunzo
ya kingereza,Halmashauri ya wilaya itaendesha semina/warsha kutoa stadi za
kufundishia masomo hayo kwa Sekondari hizo tisa zenye
walimu
wapatao
(71).
Mapunda
alisema mafunzo hayo ni nyongeza kwa walimu wote waliopo katika Shule hizo tisa
za mafunzo ya kingereza ya aina mbili,TEE-TZ itakayoendeshwa kwa ufadhili wa
ubalozi wa Marekani,(RELO-Regional
English
Language Office kwa Sh,24,158,480/-.
Katika
ufadhili wa mafunzo hayo ya TEE-TZ na RELO jumla ya Sh,169,103,698/-ndizo
zitakazotumika kwa ajili ya utekelezaji wake.
Mratibu
wa mradi huo,kutoka kampuni hiyo ya Pan African Energy,Anne Devilliers,amesema
lengo la mpango huo ni,kutaka kuwawezesha wanafunzi waelewe masomo yao kwa elimu
ya Sekondari na kuongeza viwango vya
ufaulu
katika mitihani yao ya kidato cha nne.
Devilliers akasema imebainika kwamba wapo
wanafunzi waliowengi wamekuwa hawafanyi vizuri katika masomo na mitihani
yao,kutokana na kutoielewa vyema Lugha ya Kingereza.
Mkuu wa
wilaya hiyo ya Kilwa, Abdallah Ulega, ameipongeza kampuni ya Pan African
Energy,na akasema kwamba kwa kiasi furani itasaidia kuboresha kiwango cha elimu
ndani ya wilaya hiyo,mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mpango
huo,ulianza kwa majaribio katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani,mwaka 2010 na
2011,baada ya kuona mafanikio yake,ndipo uongozi wa wilaya ya Kilwa,ukaamua
mpango huo kupelekwa ndani ya wilaya yao.
Post a Comment