Mh. Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akimsalimia mtoto Abrahamu Omari (miezi 3) ambaye amebebwa na mama yake
mwenye ulemavu wa ngozi anaitwa Amina Fadhilinyuma ya waziri mkuu ni Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP Reginali Mengi ambaye ndiye alianda chakula kwa walemavu
katika kukaribisha mwaka mpya 2013.
Mh
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa anasalimiana na Redds Miss Tanzania Brigiter
Alfred amabaye alikuwa ni miongoni mwa wageni walikwa katika kushiriki chakula
cha mchana na walemavu kilichoanadaliwa na Mweyekiti wa Makampuni ya IPP Mzee
Mengi Picha na Chris Mfinanga
Mh
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia walemavu walio alikwa katiaka cha mchana
kilicho anadaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Reginali Mengi katika
kukaribisha mwaka mpya wa 2013 waziri mkuu alikuwa mgeni rasimi katika hafla
hiyo Picha na Chris Mfinanga
…………………………………………………….
WaZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema suala la uchangiaji wa VICOBA kwa ajili ya watu wenye
ulemavu linahitaji kupangiwa mkakati maalum ili zipatikane fedha za kutosha
kuwapa mitaji nao pia wajitegemee.Amesema yuko tayari kukaa na
Mkurugenzi Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi ili wabungue bongo ya jinsi ya
kutunisha mfuko wa VICOBA kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Ametoa ahadi hiyo leo
mchana (Jumapili, Januari 20, 2013) wakati akizungumza na watu wenye ulemavu wa
mkoa wa Dar es Salaam katika hafla yao ya chakula cha mchana ya kuukaribisha
mwaka mpya 2013 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na Bw. Mengi.
“Bwana Mengi amewasha moto
mzuri kwa kuwachangia hawa watu sh. milioni 100. Nimeambiwa kuwa walianza kwa
kujichangisha sh. milioni 17. Najua nami nawajibika kuwachangia lakini itabidi
nikae naye tuone jinsi huduma hii inavyoweza kusambaa na kuwafikia Watanzania
wengi zaidi,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema ili uwe mpango
endelevu, wabuni mpango utakaowajumuisha Watanzania wengi zaidi, wakiwemo
wanasiasa, viongozi wa dini na wengine wengi. “Nia yetu ni kila mwenye nacho
achangie ili kuwasadia wenzetu wawe na miradi ya kujikimu kimaisha kupitia
mikopo ya VICOBA,” alisema.
Akijibu risala ya watu
wenye ulemavu iliyosomwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye
Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Bi. Lupi Maswanya ambayo ilikumbushia ombi la
kupatiwa Ofisi ya kudumu, Waziri Mkuu alisema ahadi yao bado anaikumbuka,
hajaisahai ila bado naifanyia kazi.
Katika risala yao, watu
wenye ulemavu pia waliiomba Serikali iharakishe kutoa kanuni za Sheria Na. 9 ya
mwaka 2010 ya Haki za Watu wenye Ulemavu ili kuharakisha muundo wa Baraza la
walemavu na kamati zake.
“Pia tunaiomba Serikali
itohoe kwa lugha nyepesi na kuitangaza sheria hiyo katika vyombo mbalimbali
ikiwemo kuiweka kwenye maandishi ya nukta nundu kwa ajili ya watu wenye uoni
hafifu,” ilisema sehemu ya risala yao.
Pia walimuomba Rais Jakaya
Kikwete amteue Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Taifa la Watu wenye Ulemavu
ili kuharakisha uundwaji wa Baraza na Kamati zake kwa mujibu wa sheria
hiyo.
Mapema akimkaribisha Waziri
Mkuu kuongea na hadhara hiyo, Bw. Mengi aliiomba Serikali iangalie uwezekano wa
kukabili tatizo la dawa za kulevya kwa namna ya pekee kwani linachangia kwa
kiasi kikubwa tatizo la watu wenye matatizo ya akili nchini. “Hawa nao wanageuka
kuwa watu wenye ulemavu wa akili,” alisema.
Naye muasisi wa VICOBA
nchini, Bi. Devotha Likokola alisema kikundi cha watu wenye ulemavu kimefikisha
wanachama 150 lakini kinakabiliwa na changamoto ya waombaji wengi wenye ulemavu
hasa kutoka mikoani.
“Mfuko huu waliuanzisha wao
wenyewe, na kuamua kukopeshana ili wafanye biashara. Bw. Mengi akawaongezea sh.
milioni 100. Wamesema wakiwezeshwa wanahitaji miaka mitano tu nao wataanza
kufadhili watu wengine,” alisema Bi. Likokola.
Post a Comment