Kiemba, shujaa wa Simba leo |
Na Nurat
Mahmoud, Muscat
SIMBA SC
imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika ziara yake ya Oman jioni hii, baada
ya kuifunga Ahly Sidab kwenye Uwanja wa Sidab mjini
Muscat.
Katika
mchezo huo, shujaa wa Simba, alikuwa ni kiungo aliyerudi juu kisoka hivi sasa,
Amri Ramadhan Kiemba aliyeifungia timu hiyo bao la
ushindi.
Katika mechi
hiyo nzuri na ya kusisimua, wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kipindi
cha kwanza, lililofungwa na kiungo Mbrazil, aitwaye Lopez, kabla ya kiungo wa
Simba, Kiggi Makassy kusawazisha kipindi hicho hicho cha
kwanza.
Hadi
mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na leo Simba walicheza soka
nzuri mno, huku wachezaji vijana, Miraj Adam, Abdallah Seseme, Haroun Chanongo
na Shomari Kapombe waking’ara zaidi.
Kipindi cha
pili, kocha Mfaransa, Patrick Liewig alifanya mabadiliko, akiwaingiza Rashid
Ismail, Marcel Kaheza wote waliopandishwa kutoka timu B na Kiemba ambao
waliongeza makali ya Mnyama na hatimaye kupata ushindi
huo.
Alikuwa ni
kiungo wa zamani wa Kagera Sugar, Yanga SC, Miembeni na Moro United aliyeipatia
Simba ushindi wa kwanza katika ziara yake ya Oman kwa kufunga bao safi la
ushindi dakika za mwishoni.
Huo ulikuwa
mchezo wa tatu kwa Simba katika ziara hiyo, awali ikifungwa 1-0 na U23 ya Oman
na baadaye 3-1 na timu ya Jeshi la nchi hiyo, Qaboos, bao la Wekundu hao wa
Msimbazi, likifungwa na Haruna Moshi ‘Boban’.
Huo ulikuwa
mchezo wa sita kwa Mfaransa, Liewig kuiongoza Simba tangu aanze kazi mapema
mwezi huu, awali akishinda mechi moja, sare mbili na kufungwa mbili.
Aliiongoza
Simba SC kuifunga 4-2 Jamhuri, sare ya 1-1 na Tusker FC, 1-1 na
Bandari zote katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar, kabla ya kufungwa 1-0 na
U23 ya Oman na 3-1 dhidi ya Qaboos katika ziara ya
Oman.
Simba SC
inatarajiwa kurejea nchini Jumatano baada ya ziara hiyo, tayari kwa mzunguko wa
pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika
mchezo wa leo, kikosi cha Simba kilikuwa; Juma Kaseja, Miraj Adam, Paul Ngalema,
Mussa Mudde, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Haroun Chanongo, Abdallah Seseme,
Abdallah Juma/Rashid Ismail, Mrisho Ngassa/Marcel Kaheza na Kiggi Makassy/Amri
Kiemba.
REKODI YA
PATRICK LIEWIG SIMBA SC
Simba SC 4-2
Jamhuri (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 1-1
Tusker FC (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 1-1
Bandari (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 0-1
U23 Oman (Kirafiki)
Simba SC 1-3
Qaboos (Kirafiki)
Simba 2-1
Ahly Sidab (Kirafiki)
Chanzo: Bin Zubeiry
Post a Comment