Waziri wa Habari,
Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za
rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma
Kilowoko (SAJUKI)kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa
leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo
imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na
kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa
nchini.
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na
michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.
“Nimepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko
na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo
ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt. Mukungara
amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote
wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi
Mungu.
Juma Kilowoko
(SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya
maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni
pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ .
Mwaka 2008 aliamua
kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two
Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua
kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza
filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata,
Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk.
Sajuki alifanikiwa
kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini.
Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa
filamu.
Sajuki alianza kuugua
mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini
India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali
iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu
kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu
aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya
utengenezaji.
Aidha hali yake
ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe
02/01/2013.
Mungu ailaze roho ya
Marehemu mahali pema peponi Amen.
Imetolewa
na:
Mkurugenzi
Idara ya
Habari(MAELEZO).
Dar es
Salaam.
2 Januari
2013
Post a Comment