MKALI
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Mohammed ‘TID Mnyama’ anajipanga
kuachia albamu yake ya tatu inayokwenda kwa jina la
‘Kiuno’.
TID
alishawahi kutamba na albamu zake mbili ikiwemo ya ‘Nyota yangu’ ambayo ilifanya
vizuri na kumtangaza katika nchi za jirani.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, TID alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo ambayo
anaamini itafanya vizuri kutokana na nyimbo zote zilizokuwepo humo kufanya
vizuri katika soko hilo.
Alisema
anawaomba mashabiki wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili kuipokea kazi hiyo
ambayo imetengenezwa kwa kufuata maadili ya Mtanzania.
“Nafurahi kwasababu kazi
zangu zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu naomba mashabiki wangu msichoke
kunisiliza kwani bado kuna vitu vizuri ambavyo nawaanndalia,” alisema
TID.
Mbali
na kibao chake cha Kiuno ambacho kinabeba jiana la albamu hiyo, TID alishawahi
kutamba na kibao chake cha ‘Nyota yangu’ ambacho kilimtambulisha na kufanya
vizuri zaidi licha ya kuwa na vibao vingi.
Post a Comment