Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Airtel, Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center- waungana kuendesha kampeni za Usalama Barabarani kupitia MPINGA CUP

 

Meneja Uhusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando akiongea wakati wa kutangaza kuanza kwa mashindano na kukabidhi vifaa vitakavyotumika katika mashindano yatakayo shirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda  yanayoitwa “ mpinga Cup” yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa bodabora jijini Dar es Saalam .  katikati ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga, akifatiwa na mwakilishi wa  Meneja Uendeshaji Home Shopping center Yahaya Zuludi  na Mwakilishi wa Rotary club  Dar es Saalam Vinay Choudary ambao pia ni wadhamini wa michuano hiyo. makabidhiano yamefanyika leo katika ofisi kuu ya trafiki Dar es salaam
Meneja Uhusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando akimkabidhi  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga jezi zitakazotumika katika michuano ya mpinga cup itakayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza idadi ya ajali za  barabarani .  michuano ya hiyo pia imedhaminiwa na Rotary Dar es Saalm, Home shopping center pamoja na Mr Price na  itafanyika kwa muda wa wiki nzima,  wakishuhudia katikati  ni Meneja uendeshaji Home shopping center Yahaya Zuludi na  kulia Mwakilishi wa Mr. Price Sudhirm Maharaj.makabidhiano yamefanyika leo katika ofisi kuu ya trafiki Dar es salaam
Meneja Uhusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando akimkabidhi  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga mipira itakayotumika katika michuano ya mpinga cup itakayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani . wadhamini wengine wa Mping cup ni pamoja na Rotary Dar es Saalm, Home shopping center pamoja na Mr Price . wakishuhudia katikati  ni Meneja uendeshaji Home shopping center Yahaya Zuludi na  kulia Mwakilishi wa Mr. Price Sudhirm Maharaj. makabidhiano yamefanyika leo katika ofisi kuu ya trafiki Dar es salaam
 Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akionyesha jezi zitakazotumika katika michuano ya mpinga cup itakayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda. 
 
Mwakilishi wa Mr Price Sudhirm Maharaj akikabidhi jezi kwa Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga zitakazotumika katika michuano ya mpinga cup itakayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani . michuano ya hiyo pia imedhaminiwa na Airtel, Rotary Dar es Saalm, Home shopping center pamoja na Mr Price.
     PRESS RELEASE:
           UDHAMINI WA MASHINDANO YA BODABODA –‘‘MPINGA CUP’’
Airtel, Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center- waungana kuendesha kampeni za Usalama Barabarani kupitia MPINGA CUP
Wadhamini mashindano ya mpira wa Miguu kwa waendesha bodaboda kwa lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani .Wakabidhi vifaa vya michezo vikiwemo Mipira, jezi, fulana pamoja na zawadi ya mshindi 
Dar es salaam Airtel kwa kushirikia na Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani imeibuka na mpango wa kipekee kupitia mchezo wa mpira wa miguu kwa madereva wa bodaboda utakaowakutanisha pamoja waendesha boda boda wa jijini Dar es salaam ili kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti  ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii. 
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema “ Airtel tumeona ni vyema kuendeleza ushirika wetu na Jeshi la Polisi  usalama  Barabarani  wakati wote wa mwaka  ili kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa”.Udhamini wetu katika mashindano haya ya waendesha Bodaboda una lengo la  kulinda afya za  Watanzania wanaotumia usafiri wa boda boda, kupitia ushiriki wetu tutafikisha ujumbe na elimu kwa watumiaji wa barabara kwa kuwa  michezo inaleta hamasa, inaleta burudani , inafanya mwili kuwa imara hivyo kufikiri vyema, hivyo basi ni matumaini yetu baada ya wiki  nzima ya mashindano ya mpira wa miguu washiriki hawa pia wataweka kukumbuka ya waliojifunza muda kwa kipindi cha wiki nzima kwa kutii sheria bila  shuruti  wanapofanya shughuli zao” aliongeza Bw. Mmbando
Naye Mwakilishi wa Mwakilishi wa Rotary club  Dar es Saalam Vinay Choudary alisema “Tumejipanga kupitia michuano hii  kusambaza ujumbe juu ya athari kubwa  inayoweka hatarini maisha ya waendesha pikipiki. Tunaamini elimu ya kutosha ikitolewa kwa vijana wetu wanaofanya biashara za usafiri kwa njia ya pikipiki kutawaepusha na athari hizi si tu kwa madereva bali kwa abiria na watumiaji wa usafiri huu kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akizungumziazoezi hili aliwashukuru wadau  hao  kwa kuunga mkono jitihada za serikali  za kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa asilimia tano (10%)  mwaka huu.
“Tunaendelea na mikakati mbalimbali tuliojiwekea katika kuhakikisha tunapunguza ajali za barabarani nchini. Mashindano haya ya waendesha Boda boda ni moja ya njia tunayoitumia ya kuwafikia walengwa na kutoa elimu kwa waendesha pikipiki” alisema Kamanda Mpinga. 
“Hii ni nafasi ya kipekee kwetu kuwaweka watumiaji wa barabara karibu ili tuweze kufikia malengo yetu” alisisitiza kamanda Mpinga .Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka  2012 kulitokea ajali za pikpiki 5763, vifo 930 na majeruhi 5532. Hili ni ongezeko la ajali kwa 7.0%,  upungufu wa vifo kwa 1.6% na ongezeko la majeruhi kwa 0.5%  ikilinganishwa na mwaka  2011 ambapo kulitokea ajali za pikipiki 5384 zilizosababisha vifo 945 na majeruhi 5506.  Kiwango hiki nikikubwa na kimeleta maafa na hasara  kubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla. Tunawashukuru sana Airtel , Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center  wadau  kwa kuendelea kushirikiana nasi kuhakikisha tunapunguza kabisa tatizo hili.Pia tunawashukuru wachezaji kwa timu zao waliojitokeza kupata elimu na kushiriki mashindano haya kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa. 
Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe 28/02/2013 katika viwanja vya Polisi Oysterbey   kwa kushirikisha timu 8 zote kutoka wilaya ya kinondoni ambapo ni muunganiko wa wacheza soka ambao ni waendesha pikipiki toka vituoni (vijiwe ) vya kinondoni. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.
Kampeni hizi za Usalama barabarini zitaendelea mfululizo hadi mwisho wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama barabarani hapo mwezi September/Octoba 2013
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top