Suma na Asha wakiwa hoi baada ya kufikishwa wodi
namba 3 hospital ya mkoa wa Morogoro,baada ya kiwanda cha kutengeneza nguo za
Michezo cha Mazava kilichopo Msamvu mkoani hapa kupata hitiafu ya umeme leo
asubuhi
Mmoja wa mareuhi hao akiwa hoi wodi namba 3
hospital ya mkoa wa Morogoro
Muuguzi
akimuhudumia Bi Nyamile Matai
Baadhi ya Ndugu na jamaa wa wafanyazi ho ambao baada
ya kupata taarifa hizo walifurika hospital ya mkoa wa Morogoro na kuwashuhudia
ndugu zao kupitia madirishani kama walivyonaswa
Majerehi huyo jina lake halikupatikana kutokana
na hali yake kuwa mbaya
Wauguzi wakiwahudumia majeruhi hao wa kiwanda cha
Mazava Everin Misaki[kulia] na Dotto Jumanne
Bi Asha Ally akiwa hoi wodi namba 3
hospital ya mkoa wa Morogoro
Bi, Subira Juma Athumani[kushoto] akiwa na majeruhi
wenzake ambao waligoma kutaja majina yao na kupigwa picha.
KWA mara
nyingine tena zaidi ya wafanyakazi 50 wa kiwanda cha kutengeneza nguo za Michezo
cha Mazava kilichopo maeneo ya Msamvu mkoani hapa wamelazwa hospital ya rufaa ya
mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufutia shoti ya umeme iliyo tokea leo
majira ya saa 4 asubuhi.
Kumbukumbu za
Mtandao huu zinaonyesha hii ni mara ya tatu wafanyazi wa kiwanda hicho ambao
wafanmyakazi wengi ni wanawake kukumbwa na tukio kama hili nakwamba kwa bahati
nzuri hakuna mtu aliyelipotiwa kupoteza maisha ingawa baadhi yao hali zao sio
nzuri.
Kufuatia hali
hiyo Mtadao huu ulifukunyua fukua baada ya kuwapiga maswari ya mitego majeruhi
hao ambao baadhi wamekili kwamba hali hiyo inayojiludia mara kwa mara inatokana
na hujuma za baadhi ya wafanyazi wanaolalamika kufanya kazi kwa masaa 12 kwa
mashahara ya shilingi elfu 80.
Vile vile
katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya vigogo wa kiwanda hicho waliwazuia
wafanyazi wa kikosi cha zima moto, Tanesco na waandishi wa habari kuingia ndani
ya kiwanda hicho wakidai kwamba hakuna tukio lolote kubwa lililosababisha
taasisi hizo muhimu kuingia ndani ya kiwanda hicho.
Kwa habari
zaidi na picha za tukio hili,na hujuma zilizotajwa endela kutemebea mtandao huu
ambao kwa sasa uko ndani ya hospital hiyuo ukizidi kuchimba chimba hujuma
hizo.
NA DUSTAN
SHEKIDELE,MOROGO.
Post a Comment