Mhe. Balozi Peter Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa mgahwa wa FORODHANI ulipo Barking pamoja baadhi ya watanzania na viongozi wao alipo watembelea Jumamosi iliyo pita |
Wafanyabiasha
Wakitanzania washio jiji la London siku ya Jumamosi, tarehe 23, mwezi 2
walitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe.
Lengo la
ziara hiyo ni kubadilishana nao mawazo na kuangalia jinsi gani
wafanyabiashara hao wanavyoweza kutumia fursa za kiuchumi zinazojitokeza
nchini Tanzania.
Katika
ziara hiyo wafanyabiashara hao walimueleza Balozi Kallaghe mafanikio yao
na changamoto zinazowakabili kwanye uendeshaji wa shughuli zao za kila
siku.
Wafanyabiashara
waliotembelewa ni pamoja na Bi. Jennifer Wright anayemiliki biashara ya
kuuza na kununua nyumba pamoja na Soloon za nywele, Bw. Augustino Msey
mwenye kampuni ya Swahili Travel and Tours, Moona Store (dukani kwa
Sadi) wauzaji wa vifaa vya umeme na wakala wa Westen Union, Salumu wa
Barking anayemiliki Foro Barbeque Food, na pia Balozi Kallaghe alipata
fursa ya kuhudhuria uzinduzi wa kikundi cha jamii cha Istiqama UK.
Balozi Kallaghe aliambatana na wanajumuia ya Kitanzania Bw. Haruna Mbeyu
na Bi. Mariamu Mungula.
Balozi
Kallaghe alipokutana na mmoja wa wafanyabiashara Bi. Jeniffer Wright
alisema kuwa yupo tayari kuwasaidia Watanzania waishio Uingereza na
waliokuwepo nyumbani kwa kuwapa mafundisho na maelekezo ya kibiashara
kutokana na ujuzi aliokuwa nao. Pia Bi. Wright aliomba serikali ya
Tanzania ipunguze vizuizi vya biashara ili waweze kuwekeza nchini
Tanzania. Nae Mwenyekiti wa Swahili Group Bw. Augustino Msey alisema
kuwa kampuni yake inajitahidi kuitangaza Tanzania katika sekta ya
utalii. Bw. Msey aliendelea kusema kuwa kampuni yake inafanya mikakati
mikunbwa ya kuwekeza nchini Tanzania. Vilevile Forodhani Barbeque Food
waliomba serikali waliangalie suala zima la uraia pacha, kwani
Watanzania wanapata tabu sana na vizuizi vingi wanapotaka kuwekeza
nchini.
Balozi
Kallaghe aliwashauri Watanzania wote wajumuike kwa pamoja, na
washirikiane kuleta maendeleo na kuwekeza nchini Tanzania na vilevile
wanapopata matatizo wasisite kwenda ubalozini kutaka ushauri na kuomba
msaada.
Post a Comment