Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mama kikwete atoa msaada rufiji

 


001.IKWIRIRI 51a44
. Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete(katikati) pamoja na Mganga
Mkuu wa Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani Bw.Haruna
Mhina,wakipokea msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka
kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
 
004.IKWIRIRI 41b19
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake
na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,mara baada ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya
tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa
eneo Nyamisati iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani.
005.mama 9959d
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea na baadhi ya wakazi wa Nyamisati
wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa
vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo
wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.
006 a61db
 Baadhi ya wakazi wa Nyamisati wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mke wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,
WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea nao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano
ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya
Nyamisati, iliyopo wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.

 
Mama Kikwete akabidhi msaada wa vifaa vya tiba Rufiji
Rufiji-Pwani,Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete, amewaasa wakazi
wa Nyamsati, mkoani Pwani kuweka mambo ya kisiasa na vyama vyao pembeni na
badala yake kushikamana kwa pamoja na kujenga Taifa alisema hayo wakati wa kukabidhi
msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20, kwenye Kituo cha
Afya cha Nyamsati, mkoani Pwani, uliotolewa na Mfuko wa Huduma za Jamii wa Vodacom
Tanzania(Vodacom Foundation)
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika hapo jana, katika Kituo cha Afya cha Nyamsati
mkoani hapa, ambapo pamoja na mambo mengine, mama Kikwete ameishukuru Vodacom
Foundation kwa msaada huo, nakutoa rai kwa wadau wengine kujitokeza na kuunganisha
Nguvu katika kukabiliana na matatizo ya kijamii,hasa eneo la afya ya mama na mtoto.
“Idadi ya vifo vya mama na mtoto, mapambano dhidi ya Malaria na UKIMWI, chanjo
kwa watoto ikiwemo ya ugonjwa wa Nimonia, mimba kwawanafunzi wa kike pamoja na
kuwawezesha wajasiriamaliwa kike ni mambo muhimu ambayo jamii inapaswa kuyatazama
kama changamoto na kuangalia namna ya kukabiliana nayo,” amesema.
Mama Kikwete amesema upungufu wadawa na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya
na hospitali nchini bado ni changamoto, na kwamba msaada uliotolewa utasaidia kuunga
mkono jitihada za Serikali zenye lengo la kuleta ustawi wa huduma za Afya kwa manufaa
ya watu wa Nyamsati na mkoa wa Pwani kwa ujumla.
Akipokea msaada huo, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyamsati wilaya ya rufiji mkoa wa
pwani Bw.Haruna Mhina alisema Kituo hicho cha afya ambacho kinahudumia wastani ya
wagonjwa 2000 kwa mwezi kinakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madawa
na vifaa tiba lakini kupitia msaada huo, kwa kiasi kikubwa utasaidia kutatua ukubwa
watatizo hilo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mfuko wa Kusaidia Jamii wa Vodacom,Bw.
Yessaya Mwakifulefule, amesema kuwa mfuko huo siku zote umekuwa mstari wa mbele
kushirikiana na taasisi na vituo kadhaa vya afya nchini katika kukabiliana na changamoto
zinazoikabili sekta ya afya nchini kupitia misaada mbalimbali wanayoitoa.
“Azma ya Vodacom nikuhakikisha tunaifikia jamii na kushirikiana nayo katika kukabiliana na
changamoto zinazoizunguka kwenye maeneo yote,hususani afya na elimu, na tutaendelea
kuisaidia Nyamsati kadiri itakavyowezekana ili kuleta ustawi mzuri kwa afya ya watu wake,”
amesema Mwakifulefule
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top