Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BLOG YA KAMANDA KAMANDA WA MATUKIO YALAMBA TUZO LA KONGAMANO LA NHIF

 

Mmiliki wa Blog ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akionesha tuzo ya cheti aliyopatiwa na Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kwa kutambua mchango wake katika masuala ya mfuko huo, wakati wa Kongamano la NHIF na Wanahabari la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari katika halmashauri 26 nchini kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya Afya. Kongamano hilo lililoshirikisha wanahabari 150  lilimalizika mwishoni mwa wiki Mjini Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Kalmbo, Moshi Chang'a (katikati) akimkabidhi tuzo hiyo Mmiliki wa Blog ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.
Mmiliki wa Blog ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda (katikati), akiwa na wanahabari wenzie wakati wa Kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamini Mkapa katika Chuo cya Ualimu Mtwara, mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni; Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile, Mtangazaji wa Televisheni ya ITV Mara, George Marato, Mtangazaji wa ITV, Dar es Salaam, Godfrey Monyo.
 
Credits: Sufiani Mafoto
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top