Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo
pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola
kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela
pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi
zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola,
serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la
Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti z\ilizofanywa
na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya
masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini.
Meneja wa
Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas
Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma nchini, wakati wa
Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti
zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi
kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo
lilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa
zinauzwa nje ya nchi ikiwemo Cameroon.
Msajili wa
Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati ya usajili
wa maduka ya dawa baridi vijijini wakati wa kongamano hilo.PICHA NA KAMANDA WA
MATUKIO
Post a Comment