Picha ikionesha
heliKopta ikiwa inapeleka chakula na maji kwa waanga walioshindwa kushuka kwa
kutumia miamvuli maalum katika mlima kilimanjaro
******
Marubani waliopanda mlima
Kilimanjaro kwa ajili ya kuruka kutoka kileleni kwa kutumia miamvuli maalum
wanaendelea kusota baada ya hali mbaya ya hewa kuwazuia kutekeleza azma
yao.
Wakiwa wametimiza siku 11
sasa tangu waanze safari yao mlimani, inaripotiwa kuwa hivi sasa wameanza
kuishiwa akiba ya chakula na helikopta iliyosheheni maji na shehena nyingine ya
vyakula imeruka kwenda kileleni siku ya Jumatano ili kuvidondosha kwa wahanga
hao.
Marubani hao zaidi ya 100
walikuwa wanatarajiwa kuruka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa kutumia
miamvuli maalum (Paragliding)na kutua eneo la Kibosho siku ya Jumanne, lakini
hadi leo hii (Alhamisi) bado wako mlimani.
Mkuu wa Hifadhi ya Mlima
Kilimanjaro Erastus Lufungulo amesema hali ya hewa mlimani hapo bado inaendelea
kuchafuka kwa upepo mkali na mawingu mazito.
Marubani hao wa kimataifa,
wanatoka nchi mbalimbali duniani, walitarajiwa kuwa binadamu wa kwanza kabisa
kuruka kutoka kilele hicho kirefu zaidi barani
Afrika.
Helikopta maalum ilitumwa
mara kadhaa kuzunguka mlimani kwa siku mbili mfululizo ili kujaribu kuona
marubani hao 100 wakiwemo wanawake 30 watakuwa wamefika wapi. Na siku ya jumanne
usiku, watu 15 waliokuwa kwenye timu hiyo walirudishwa chini na kukimbizwa
hospitali baada ya kuugua.
“Ni kweli zoezi
limeshindikana hadi sasa ila hatuna wasiwasi na usalama wa watalii hao kwani
tumekwisha kujiandaa kwa huduma zote za uokoaji,” alisema Afisa Habari wa
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Paschal
Shelutete.
Shelutete amesema hii ni
mara ya kwanza kabisa tukio hili la kuruka kutoka kilele cha Kilimanjaro kwa
kutumia miamvuli kufanyika nchini na kwamba likifanikiwa litajumuishwa kuwa
miongoni mwa vivutio vipya vya utalii.
Marubani hao walianza
kupanda mlima tarehe 27 Januari na ilitarajiwa kuwa wangeruka kutoka kilele cha
Uhuru siku ya tarehe 5, wakielea kutumia miamvuli hiyo maalum, ikiwa ni tukio la
kwanza kabisa kufanyika nchini.
Mratibu wa taasisi ya
‘Wings of Kilimanjaro,’ ya Australia, inayoratibu zoezi hilo, Bi Paula McRae
amesema zoezi hilo pia litasaidia kuchangia fedha kiasi cha dola millioni moja
za kimarekani kwa ajili ya kusaidia jamii zinazounguka mlima huo mrefu zaidi
barani Afrika.
Picha ikionysha mwanamama
aliyekuwa katika hali mbaya na kuamua kulala chini huku akimhofia mumewe
alipanda mlima mara baada ya kupata taarika kuwa hali ya mlima huo bado ni
tete
Hapa ni baada ya heliKopta
kurudi chini ambapo kamera ilifungwa na baadae kuleta hali halisi ya mlima huo
…..hapa ndugu jamaa na marafiki wa marubani wakiwa wanaangalia video ya tukio
hilo
Kikosi kazi cha waandishi
wa habari walioweka kambi maalum kuwasubiri watalii kushuka kutoka mlima
Kilimanjaro kwa kutimia miamvuli,zoezi ambalo halikuzaa
matunda
Post a Comment