Ramadhan Shauri |
FEBRUARY 6,
2013
DAR-ES-SALAAM,
TANZANIA
Bingwa wa IBF katika bara
la Afrika uzito wa unyoya (Featherweight) Ramadhani Shauri amepewa nafasi ya
kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana walio chini ya miaka 25 uzito wa
Lightweight. Shauri ambaye alishinda taji la ubingwa wa IBF katika bara la
Afrika mwaka jana baada ya kumpiga bondia Sunday Kizito wa Uganda ana rekodi ya
mapambano 17.
IBF imeamua kumpatia Shauri
nafasi ya kugombea ubingwa huo wa dunia kwa vijana baada ya kuangalia mkanda wa
video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa anaweza kushindania
ubingwa huo wa vijana,
Mabondia wengi wa Marekani
ambao walikuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza kupata pesa nyingi walianza kuwa
mabingwa wa dunia kwa vijana na hivyo kuweza kupanda chati kwenye viwango vya
IBF. Mbondia hao ni kama Bernard Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la
Hoya.
Kama Shauri atashinda na
kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa
duniani kama kina Dong King, Bob Arum na wengine wengi. Nafasi kama hii inaipa
nchi ya Tanzania nafasi nzuri sana ya kujitangaza kibiashara na utalii kwani
dunia inaiona kuwa kati ya nchi zinazotoa mabingwa wa
dunia.
Kama Shauri atashinda taji
hili atakuwa Mtanzania wa kwanza tangu historia ya ngumi nchini kuweza kushinda
taji la shirikisho kubwa kati ya manne duniana ambayo ni IBF, WBA, WBO na
WBA.
Shiriksiho la Ngumi la
Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo lina makao yake makuu ya kuhudumia bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ndilo lililomtafutia Shauri nafasi
aliyopata.
IBF/Africa inawahamasisha
Watanzania walio na mapenzi mema na nchi yao pamoja na makampuni mbalimbali
bifsi ya umma yajitokeze kwa wingi kumpatia Shauri ufadhili wa kuweza kuligombea
taji hili.
Mungu mbariki bondia
Ramadhani Shauri, Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amen.
Imetolewa
na:
UTAWALA
Shiriklisho la Ngumi la
Kimataifa Afrika (IBF/Africa)
Dar-Es-Salaam,
Tanzania
Post a Comment