Mwenyekiti wa kamati ya
TWAA Bi Sadaka Gandi akiongea na Waandishi wa Habari Leo
----
DAR ES SALAAM,
TANZANIA, – Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) imezindua Tuzo za
Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika
siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo
hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya
wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia
kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au
nyingine.
"TWAA inataka kutambua
wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio
makubwa sit u kibinasi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko
ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi.
Irene Kiwia. "Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa
nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye
kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara
ya kwanza mafanikio na michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufajiri na
kuridhisha sana.”
Vipengele vya tuzo za
mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na
Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi
na Teknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.
Bi Sadaka Gandi,
mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama,
wanawake na wanaume kote Tanzania kuteua wanawake wenye mafanikio katika makundi
haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya
wanawake wastahili wa tuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wa mabadiliko katika
jamii zao. Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya
wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta
mabadiliko. Kamati ilipokea fomu za nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na
hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "
Kamati ya TWAA
inawajumuisha Bi Mary Rusimbi - Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya
Mtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello - Kamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga- Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo – Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID,
Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi - Mwanasaikolojia na mfanyakazi za
Jamii, Irene Kiwia - Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano
ya jamii Frontline Porter Novelli. Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na
Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, Watu wa Marekani,
DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life
Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na
Frontline Porter Novelli.
KUHUSU TANZANIA WOMEN
OF ACHIEVEMENT (TWA)
TWA ni taasisi isiyo ya
kiserikali, ya hiari na kujitegemea inayojihusisha na uwezeshaji wa wanawake
iliyoanzishwa mwaka 2009. Lengo kuu la TWA ni kuimarisha ushiriki, na majukumu
ya wanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mabo ya kijamii,
kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. TWA inafanya kampeni, mafunzo, semina,
mikutano na warsha ambazo zinakuza ubadilishanaji wa taarifa na ushauri kwa
wanawake na wasichana wadogo wa Kitanzania.
Kampeni na mafunzo haya
yanalenga zaidi haki za binadamu na za wanawake, usawa wa kijinsia, ushiriki wa
wanawake kweye shughuli za kiuchumi na kijamii.Kazi kubwa ya TWA ni kuboresha
maisha, kupanua fursa, na kuwasaidia wanawake katika Tanzania kushamiri na
kuchangia kwenye ustawi wa nchi. TWA inafanya kazi na viongozi ,watu binafsi,
jamii, mashirika yasiyo ya kiserekali, serikali, sekta binafsi na wafadhili wa
nje kujenga ufanisi na kuhakikisha malengo ya kuendeleza wanawake yanafanikiwa.
Sisi ni kosa kwa maendeleo ya Tanzania kuendelea mpaka kila mwanamke anakuwa
mabadiliko. Tumejikita kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea na wanawake ni
chachu ya maendeleo hayo.
Post a Comment