Afisa
Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) akimkabidhi hivi
karibuni katika ukumbi wa Karimjee zawadi ya redio (music sytem)
Winfrida Leonard kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA –
Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani ambaye alishika nafasi ya tatu
katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa
vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi
wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya
wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki.
Faiza
Ussi kutoka shule ya Sekondari ya Sunni Madressa ya mjini Zanzibar
alifurahia zawadi ya laptop aliyopewa hivi karibuni katika ukumbi wa
Karimjee mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya
kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania.
Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania
waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32
kutoka shule nane walishiriki.
Meneja
wa shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama Ali Mindria
(kulia) akipokea kombe la ushindi hivi karibuni katika ukumbi wa
Karimjee kutoka kwa Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda
(kushoto) baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika shindano
la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania
lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa
ufadhili wa Japan (JATA). Wanafunzi wane kutoka shule hiyo waliingia
kumi bora kwa kushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa kati ya
wanafunzi 32 walioshiriki shindano hilo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakiwa katika
picha ya pamoja hivi karibuni na wanafunzi wanne kutoka shule ya
Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama walioshiriki shindano la
kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania
lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa
ufadhili wa Japan (JATA) nakushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa.
Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki katika mashindano hayo
yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo shule ya WAMA-Nakayama
aliibuka mshindi wa jumla.
Washindi
kumi walioshiriki shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara
yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa
Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) wakiwa katika picha
ya pamoja hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni
waalikwa waliohudhuria hafla hiyo. Wanafunzi 32 kutoka shule nane
walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza
ambapo mshindi wa kwanza alipata laptop yenye thamani ya dola 600 za
kimarekani. (Picha na Anna Nkinda – Maelezo).
Post a Comment