Leo hii, Wabunge mbalimbali, miongoni mwao wa
kutoka CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini
Dodoma baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuikataa hoja ya Mbunge wa
kuteuliwa, James Mbatia ya iliyomtaka
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa kuwasilisha nakala za Mtaala wa Elimu za mwaka 2005.
Mitaala hiyo iliombwa tangu kikao cha Bunge lililopita na
serikali iliahidi kuileta bungeni lakini baada ya Mh. James Mbatia kuombwa
ahitimishe hoja yake binafsi na kukumbushia ahadi hiyo na kisha kuiomba serikali
kuigawa mitaala hiyo kwa wabunge, Naibu Spika Job Ndugai alisema atatafakari
ombi hilo na akiona linafaa, ataitaarifu Serikali na kuileta Bungeni. Akamtaka
Mhe. Mbatia ahitimishe hoja yake.
Mbatia akaomba aliomba mwongozo wa
Spika lakini ghafla Naibu Spika alimwabia muda wanaoutumia kuombea miongozo ndio
muda wake wa kuhitimisha hoja.
Mbatia akalieleza Bunge kuwa jana
alimwandikia Waziri wa Elimu kuwa anaiomba Mitaala hiyo lakini hakupata jibu,
alishakwenda Wizara ya Elimu kuomba mitaala hiyo lakini hakupewa, ndipo
alipohoji, “ikiwa Mbunge anadanganywa kiasi hiki itakuwaje kwa Mtanzania wa
kawaida?”
Wabunge wa CHADEMA waliungana na wale wa NCCR-Mageuzi katika
kuibana serikali. Naibu Spika, Ndugai aliwakwepa na kusema yeye ndiye mwenye
maamuzi ya kuiomba serikali au la.
Ndugai akahitimisha hoja ya Mbatia na
kutoa fursa ya kusikilizwa kwa hoja ya Dk Hamisi Kigwangallah, ndipo wabunge wa
walipoamua kutoka nje ya ukumbi wa
Bunge.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kuwasilisha nakala za Mtaala wa Elimu za mwaka 2005.
Mitaala hiyo iliombwa tangu kikao cha Bunge lililopita na serikali iliahidi kuileta bungeni lakini baada ya Mh. James Mbatia kuombwa ahitimishe hoja yake binafsi na kukumbushia ahadi hiyo na kisha kuiomba serikali kuigawa mitaala hiyo kwa wabunge, Naibu Spika Job Ndugai alisema atatafakari ombi hilo na akiona linafaa, ataitaarifu Serikali na kuileta Bungeni. Akamtaka Mhe. Mbatia ahitimishe hoja yake.
Mbatia akaomba aliomba mwongozo wa Spika lakini ghafla Naibu Spika alimwabia muda wanaoutumia kuombea miongozo ndio muda wake wa kuhitimisha hoja.
Mbatia akalieleza Bunge kuwa jana alimwandikia Waziri wa Elimu kuwa anaiomba Mitaala hiyo lakini hakupata jibu, alishakwenda Wizara ya Elimu kuomba mitaala hiyo lakini hakupewa, ndipo alipohoji, “ikiwa Mbunge anadanganywa kiasi hiki itakuwaje kwa Mtanzania wa kawaida?”
Wabunge wa CHADEMA waliungana na wale wa NCCR-Mageuzi katika kuibana serikali. Naibu Spika, Ndugai aliwakwepa na kusema yeye ndiye mwenye maamuzi ya kuiomba serikali au la.
Ndugai akahitimisha hoja ya Mbatia na kutoa fursa ya kusikilizwa kwa hoja ya Dk Hamisi Kigwangallah, ndipo wabunge wa walipoamua kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Post a Comment