…………………………………………………………….
HATIMAYE lile Sakata la
Migogoro ya Ardhi ambayo imedumu kwa muda mrefu Wilayani Manyoni
Kufuatia Shinikizo la Wananchi kuwaondoa Maafisa Ardhi limefanikiwa
baada ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Perseko Vicent Kone Kuwasimamisha
Kazi kwa muda usiojulikana Maafisa Ardhi watatu ambao ndio walikuwa
wakilalamikiwa sana na wananchi ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri
Bi.Fotunata Marya kunusurika kutokana na uchache wa malalamiko dhidi
yake ambapo wananchi wawili tu ndio waliweza kulalamikia utendaji kazi
wake.
Katika Mkutano wa Hadhara
uliofanyika katika viwanja vya Mnadani eneo la Majengo wilayani Manyoni
ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida alikuwa katika ziara yake ya kikazi
aliwaruhusu wananchi 45 kutoa kero mbalimbali ambazo zinawakabili.
Mtandao huu uliwahi kuandika ziara
ya Mkuu wa Wilaya Manyoni Bi.Fatma Hassan Toufiq ambapo wananchi wa
eneo la Majengo na Kipondoda walimuomba kumtimua Kazi Afisa Ardhi
Leonard Msafiri kwakuwa amekuwa kero kubwa katika wilaya ambapo alikuwa
akipora viwanja vya wananchi pasipo kufuata taratibu wala kuwalipa fidia
wananchi wanaomiliki maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida katika
ziara yake ya siku tatu wilayani Manyoni akiwa katika eneo la Majengo na
kipondoda aliweza kukutana na madudu ambayo yalikuwa yakifanywa na
Maafisa ardhi ambapo wananchi 45 waliweza kutoa kero zao kuhususiana na
kuporwa meneneo yao bila kulipwa fidia na maafisa wa ardhi ambao
walikuwa wakitajwa kwa majina huku baadhi ya watoa kero wakilia kwa
uchungu na kumuomba mkuu wa mkoa kuingilia kati sakata hilo ambalo
limedumu kwa miaka mingi bila ufumbuzi.
Akijibu kero zao katika mkutano wa
Hadhara DK.Kone alisema amesikia kilio cha wananchi wa Manyoni na
kuanzia sasa “Ninasimamisha Shughuli zote za ugawaji na upimaji wa
Viwanja wilayani Manyoni mpaka pale maeneo yote yanayolalamikiwa yawe
yamepatiwa ufumbuzi,na nimesimamisha shughuli zote za ujenzi kwenye
maeneo yote yanayolalamimikiwa,na Kuanzia sasa nawasimamisha Kazi
Maafisa Ardhi wanaolalamikiwa Bw. Leonard Msafili,John Chima na Kenedi
Chigulu ambao wamesababisha malalamiko haya”.
Huku akishangiliwa na wananchi
alisema “naunda tume ya wataalamu watakaotoka Mkoani,ni tume
itakaoshirikisha wataalamu mbalimbali watakaochunguza mgogoro wote na
wanipe mapendekezo,tume hiyo inatarajia kuanza kazi Tarehe 4 Februaly
2013,itafanyakazi kwa muda wa siku saba na itwahoji wote kwani nataka
kupitia mgogoro huu wa masuala ya Ardhi utakuwa fundisho kwa watumishi
wote ambao siyo waadilifu kwani watakaofukuzwa kazi
watafukuzwa,watakaopewa onyo watapewa na watakaoburuzwa kortini
wataburuzwa bila kuonewa haya kwani muda wa kulindana umepitwa na
wakati”.alisema.
Kuhusu suala la Mkurugenzi naombeni mnipe muda.
Post a Comment