Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa ufafanuzi hali iliyotokea Bungeni leo
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
1.0 UTANGULIZI
Waheshimiwa Wabunge, tangu tarehe 30 Januari, hadi jana tarehe 4 Februari, 2013 tuliamua kuwasilisha Bungeni Hoja Binafsi za Wabunge ambazo ziliahirishwa katika Mkutano wa Tisa wa Bunge kwa nia njema ya kujadiliana masuala makubwa ya kitaifa na kuishauri Serikali nini kifanyike ili kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayowahusu Wananchi. Hata hivyo, imelazimu kuahirisha mijadala ya Hoja Binafsi kutokana na tabia iliyojitokeza ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya Wabunge na hivyo kuamua kwa makusudi kuanzisha vurugu na hivyo kulifanya Bunge lianze kupoteza heshima yake ya Kibunge.
Waheshimiwa Wabunge, siku zote nimekuwa nikisisitiza matumizi ya Kanuni za Bunge ambazo ndizo mwongozo wau endeshaji wa Bunge. Hoja Binafsi za Wabunge zinaongozwa na Kanuni za Bunge kuanzia Kanuni ya 53 hadi 58 na Kanuni za majadiliano zinaongozwa na Kanuni kuanzia 59 hadi 71 ambazo kwa ujumla wake zikifuatwa kama inavyotakiwa, vurugu haiwezi kutokea Bungeni.
Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano huu imeonyesha waziwazi baadhi ya Wabunge kwa makusudi na kwa nia ya kupotosha Wananchi wakitumia vibaya Kanuni hizi na wakati mwingine kuwadanganya Wananchi ambao kwa bahati mbaya Kanuni hizi hawazifahamu kwamba ama Kanuni hazifuatwi na Kiti au zinakiukwa. Nitatoa mifano michache kwa yale yaliyojitokeza katika hoja hizi ambazo zimejadiliwa.
2.0 UTARATIBU WA UENDESHAJI WA HOJA BINAFSI
Kanuni za Bunge zinaeleza wazi kuwa Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja Bungeni ili kupendekeza jambo lolote lijadililiwe. Pendekezo hilo linatakiwa liwe limekamilika ililipate uamuzi bayana wa Bunge [Kanuni 54(1)-(2)]. Kama Hoja inayohusika ni Hoja ya Serikali, Msemaji wa Kambi ya Upinzani atapewa nafasi ya kutoa maoni juu yaHoja hiyo, na kama Hoja inayohusika siyo ya Serikali, Msemaji wa Serikali atapewa nafasi ya kutoa maoni ya shughuli za Serikali juu ya Hoja hiyo [Kanuni 53 (6) (c)].
(1)Tumeshuhudia Mbunge analazimisha na kuhoji mamlaka ya Spika kutoa nafasi kwa Mawaziri kuzungumza mara baada ya mtoa hoja na kuonyesha kwamba hilo ni kosa hivyo kuonyesha Umma wa Tanzania Kiti kinapendelea. Kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Kanuni ya 53(6) (c) ya Bunge imewekwa bayana utaratibu utakaotumika kwenye hoja hizi kwamba kama hoja inayohusika sio ya Serikali, msemaji wa Serikali atapewa nafasi ya kutoa maoni yashughuli za Serikali juu ya Hoja hiyo.
Kanuni ya 62 ya Kanuni za Bunge imebainisha muda utakaotumiwa na waongeaji kwamba anayetoa Hoja anazo dakika thelathini na anayetoa maoni ya upande wa pili anapewa muda wa dakika thelathini. Spika hataruhusu Hoja yoyote inayokiuka Katiba au Sheria au Kanuni za Bunge na Katibu atairudisha Hoja hiyo pamoja na vielelezo vyake vyake vyote kwa Mbunge mhusika na maelezo ya sababu za kukataliwa kwa Hoja hiyo [Kanuni55(9)].
Iwapo Mbunge anapenda kufanya mabadiliko ya maneno aliyotumia katika Hoja anayokusudia kuitoa, anaweza kufanya hivyo kwa kutoa taarifa ya kufanya mabadiliko kablaau wakati wa kuwasilisha Hoja yake. [Kanuni 55(10 -11)].
Pamoja na kuwa taarifa ya kutaka kufanya marekebisho aumabadiliko itakuwa imetolewa, marekebisho au mabadilikoyoyote hayatakubaliwa kama kwa maono ya Spika yataonekana kubadilisha mambo ya msingi yaliyomo katika Hoja au yanabadili makusudio au upeo wa Hoja hiyo. [Kanuni55(12)].
Hoja ikishatolewa ili iamuliwe inaweza kubadilishwa kwa:-
a) Kuondoa maneno Fulani kwa ajili ya kuingiza maneno mengine;
b) Kuondoa maneno Fulani bila kuongeza mengine; au
c) Kuingiza au kuongeza maneno mapya. [Kanuni 57(1)]
Iwapo hoja ya mabadiliko inapendekeza kuondoa maneno fulani au kuingiza maneno mengine, basi mjadala juu ya suala la kufanya mabadiliko unaweza kuangalia kwa pamoja yale maneno yanayopendekezwa yaondolewe na maneno ambayo yanapendekezwa yaingizwe [Kanuni 57(5)];
Iwapo Hoja itapendekeza kuondoa au kuingiza maneno, mjadala utahusu tu uondoaji au uingizaji wa maneno mapya, kadri itakavyokuwa na Hoja hiyo itajadiliwa na kuamuliwa kabla ya ile Hoja ya kwanza ya mabadiliko kufanyiwa uamuzi. [Kanuni 57(6-7)].
Endapo Spika atasimama wakati Waziri au Mbunge anatoa hotuba Bungeni au atakuwa amesimama mahali pake akisubiri kuanza kuzungumza, Waziri au Mbunge huyo ataketi mahali pake na Bunge litabaki kimya ili Spika awezekutoa maelekezo au taarifa yake.
3.0 HOJA YA MHESHIMIWA JOHN MNYIKA
Kulingana na maelezo hayo ya utangulizi, Hoja ya Mheshimiwa John John Mnyika, Mbunge wa Jimbo la Ubungo ilikidhi vigezo na alipewa nafasi ya kuiwasilisha Bungeni na akawasilisha Hoja yake. Baada ya Hoja hiyo kuwasilishwa, na mujibu wa kanuni ya 53(6) (c) Waziri wa Maji ambaye ndiye msemaji wa Serikali kuhusu maudhui ya Hoja husika, alipewa nafasi ya kuwa mchangiaji wa kwanza na kutoa maoni ya Shughuli za Serikali juu ya Hoja ya Mheshimiwa John Myika.
Aidha, maoni hayo ya Waziri wa Maji yalizingatia Kanuni ya 57(1) (c) inayoruhusu kuingiza au kuongeza maneno mapya kwenye Hoja iliyotolewa. Kimsingi Mheshimiwa Waziri wa Maji aliongeza maneno katika Azimio Jipya lililoomba Hoja ya msingi iondolewe, kwa sababu alizozieleza Waziri.
Hata hivyo, kwa kuwa Kanuni za Bunge haziweki ufafanuzi wa maneno gani yatumike katika kuongeza au kupunguza maneno mapya katika kuifanyia mabadiliko hoja iliyowasilishwa, hivyo maneno yaliyoongezwa na Waziri ya kuondoa hoja hiyo yalikuwa sahihi na yalikidhi matakwa ya Kanuni za Bunge kwa kuwa yalikuwa ni sehemu ya maazimio ya hoja yenyewe ambayo iliamuliwa na Bunge kwa mujibuwa Kanuni ya 57(6-7) inayotaka hoja ya kuingiza au kuongeza maneno iamuliwe kwanza kabla ya kuendelea na Hoja ya awali.
Waheshimiwa Wabunge Kanuni ya 58 ya Kanuni za Bunge imeweka masharti ya namna ya kushughulikia mapendekezo ya mabadiliko yote kwenye hoja ya msingi na Spika amepewa mamlaka ya kuamua mpangilio atakaoona unafaaikiwa ni pamoja na kuzingatia masharti yaliyomo kwenyeKanuni ya 53 (6) (c). Katika Hoja ya Mhe. Mnyika, Mb – Ofisi ilipokea mabadiliko manne (4) ambayo yaliwasilishwa naWabunge, hivyo utaratibu na Kanuni ungefuatwa kamwe vurugu zisingejitokeza.
Waheshimiwa Wabunge, kwa masikitiko makubwa sote tulishuhudia vurugu zilizojitokeza katika Bunge hili hasa wakati wa mjadala wa Hoja Binafsi za Wabunge, kimsingi huu ulikuwa ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kutokea katika Historia ya Bunge letu. Taasisi ya Bunge inalaani vitendo vilivyojitokeza jana vilivyovunja Kanuni ya 60(2) inayokataza Mbunge kuzungumza kabla ya kuruhusiwa na Spika na Kanuni ya 60(12) inayowataka Wabunge kukaachini wakati wowote Spika anaposimama kutaka kuzungumza.
Aidha, kumekuwa kuna madai kuwa Kiti kinatoa upendeleo wa wazi kwa Serikali dhidi ya Upinzani, jambo ambalo sikweli. Hata hivyo kama maamuzi yanayofanywa na Kiti yana kasoro kanuni zinaruhusu Mbunge ambaye hakuridhika na maamuzi hayo, kukata rufaa kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 5 (4). Hivyo vitendo vya uvunjifu wa Kanuni na kusababisha fujo kumedhalilisha Kitina Taasisi ya Bunge kwa ujumla.
Katika Kikao cha dharura Kamati ya Uongozi kilichokaa jana, Wajumbe walitafakari kwa undani vurugu hizo zilizojitokezana kufikia maamuzi yafuatayo:-
(i) Kamati ilikemea kwa nguvu zote vitendo hivyo nakubainisha kwamba endapo vitaachiwa viendelee vinaweza kusababisha madhara makubwa kama kupigana ndani ya Bunge;
(ii) Kamati ilikubaliana kwamba suala hili lipelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ilichunguze na kuleta mapendekezo Bungeni kabla ya Mkutano huu wa Kumi kumalizika;
(iii) Kamati ilikubaliana kuwa Hoja zote Binafsi za Wabunge zisiwasilishwe Bungeni kutokana na utovu wa nidhamu uliokuwa umeanza ili kuzuia mwendelezo ambao ungeweza kujitokeza katika Hoja Binafsi zilizobakia kwa kulinda heshima ya Bunge.

Post a Comment