Baadhi
ya maafisa habari wa serikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Bw. Peter Millanzi
mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw.
Midradji Maez, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Shirika la Reli Tanzania
(TRL) na Bw. Abel Ngapemba, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Shiririka la
Maendeleo la Taifa (NDC).
Maafisa
Habari kutoka wizara mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha maafisa
habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya vikundi kuhusu
mafanikio na changamoto zinzoyakabili maeneo yao ya kazi wakiongozwa na
mwenyekiti wa kikundi hicho Luteni Kanali Juma Sipe, Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikali Wizara ya Ulinzi.
Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent
Mungy akiwasilisha mada kuhusu mkakati wa Mawasiliano wakati wa Kikao
kazi cha maafisa habari wa serikali kinachoendelea mjini Dodoma.
Maafisa
Habari kutoka wilaya na Mikoa mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha
maafisa habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya pamoja kuhusu
mafanikio na changamoto zinzoyakabili maeneo yao ya kazi.
…………………………………………………………………….
Habari, Picha na Aron Msigwa.
Kikao
kazi cha Maafisa habari wa Serikali kutoka Wizara, taasisi, wakala wa
serikali, mashirika ya umma, mikoa na wilaya mbalimbali nchini leo
kimeingia siku ya pili mjini Dodoma kwa maafisa hao kupata fursa ya
kujadili changamoto zinazokabili vitengo vya habari na mawasiliano
serikalini na namna ya kuzitatua.
Katika
kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo ile ya Mwongozo wa
Ofisi za Mawasiliano serikalini iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa
Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) anayeshughulikia uratibu wa
vitengo vya mawasiliano serikalini akitoa msisitizo mkubwa kwa maafisa
habari kuyafahamu vizuri majukumu yao ya kazi kwa mujibu wa taratibu za
utumishi wa umma ili kuboresha utendaji wa kazi.
Pia
maafisa hao wamepata fursa ya kujifunza namna ya kuboresha mawasiliano
serikalini kupitia mada ya mkakati wa mawasiliano (Communication
Strategy) wa kuiwezesha jamii kupata taarifa sahihi kwa muda muafaka
,mada iliyowasilishwa na Meneja mawasiliano kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy.
Katika
mada hiyo Bw. Mungy ametoa wito kwa maafisa hao kuzitumia nafasi zao
kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara ili kuwapa fursa wananchi kufahamu
yale yanayofanywa na serikalini.
Ametoa
wito maafisa hao kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari katika
kutekeleza mkakati huo kwa kuhakikisha kuwa wanatoa habari kwa umma
kupitia radio, magazeti, televisheni na mitandao ya kijamii ili kuepusha
madhara yanayoweza kusababishwa na jamii kukosa taarifa sahihi za
serikali za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.
Post a Comment