…………………………………..
JAJI
Mkuu wa ZanzĂbar Omar Othmani Makungu amesema kuwepo kwa Mahakama ya
watoto nchini kutasaidia kupunguza mrundikano wa kesi zinazowakabili
watoto mahakamani na kupatikana haki zao kwa wakati.
Jaji
Makungu ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mahakama ya Watoto Zanzibar
huko Vuga ikiwa ni shamra shamra ya siku ya Sheria duniani
inayoazimishwa Februari 7 kila mwaka.
Amesema
lengo la kufunguliwa Mahakama hiyo ni kukabiliana na changamoto ya
ongezeko la kesi zinazohusu Watoto na kuwapatia haki zao za msingi kwa
wakati.
Aidha
ameongeza kuwa Mahakama hiyo itakuwa ni mazingira rafiki kwa watoto
ambayo yatawasaidia kuweza kujieleza pamoja na kutoa ushahidi bila ya
hofu.
Jaji
Makungu amefahamisha kuwa wanatarajia kuanzisha Mahakama ya Watoto kwa
upande wa Pemba sambamba na kuweka mahakama ndogo ndogo katika kila
wilaya ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wananchi.
Nae
katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii maendeleo ya Wanawake na Watoto
Fatma Gharib Bilali amewataka wazee kushirikiana na mahakama hiyo ili
kuweza kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili watoto ikiwemo
kurekebisha tabia na kukufatilia nyendo zao.
“Maendeleo
yeyote lazima yawe na changamoto zake jamii lazima iwasaidie watoto
kuwalinda na vishawishi vya watu wabaya” alisema Katibu huyo.
Nao Wawakilishi kutoka Mashirika ya Kimataifa ya UNICEF na Save The Children wameishukuru Mahakama Zanzibar kwa ushirikano wao wa kuweza kuanzisha mahakama ya watoto ambayo itaweza kutetea na kulinda haki za mtoto na ustawi wake.
Post a Comment