Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimshika kwa furaha mtoto aliyezaliwa tarehe
5.7.2013 katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine huku mama wa mtoto huyo
Muksim Issa ,19, anayetoka katika kijiji cha Mumbu kilichoko katika wilaya ya
Lindi vijijini aliyelala kitandani akitabasamu. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na
uzito wa kilo 3.9 Mama Salma alitembelea hospitalini hapo kukabidhi vifaa vya
hospitali tarehe 6.2.2013. Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Lindi Dr. Nasoro Hamid.
PICHA NA JOHN
LUKUWI
Kikundi cha utamaduni kikiwatumbuiza waalikwa kwa ngoma
ya Tambiko inayochezwa na watu wa kabila la Wamakonde wakati wa sherehe ya
kukabidhi vifaa vya tiba kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Lindi, Sokoine, tarehe
6.2.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi na
wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine,na wananchi waliohudhuria
sherehe ya kukabidhi rasmi vifaa vya tiba kwenye hospitali hiyo tarehe 6.2.2013
huko Lindi Mjini. Waliokaa kushoto kwa Mama Salma ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa
hospitali Dr. Nicolaus Munni, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ambaye pia ni
Meya wa Lindi Mjini Ndugu Frank Magali na wa mwisho ni Mwakilishi wa Project
C.U.R.E. nchin Tanzania Bwana Makembe Kimario.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria
kukabidhi rasmi kwa vifaa vya hospitali ya mkoa wa Lindi,Sokoine, vilivyotolewa
na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Shirika la Project C.U.R.E. la nchini
Marekani. Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba. Kulia
kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya
Lindi Dr. Nasoro Hamidi akifuatiwa na Katibu wa CCM WA Mkoa huo Ndugu Adelina
Gefi na kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni.
Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 6.2.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete kwa furaha akiagana na wafanyakazi wa
hospitali ya Mkoa wa Lindi,Sokoine, viongozi na wananchi waliohudhuria sharehe
za kukabidhi vifaa vya hospitali hiyo tarehe 6.2.2013.

za kukabidhi vifaa vya hospitali hiyo tarehe
6.2.2013.
Post a Comment