Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, amtembelea hospitali ya Selian, inayomilikiwa na kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), jijini Arusha, kumjulia hali Askofu Thomas Laizer,
ambaye amelazwa kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita.
Pinda aliingia
hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa huku waandishi wa
habari wakizuiwa kuingia katika chumba hicho cha wagonjwa
mahututi.
Hata hivyo, baada ya
kutoka katika chumba hicho, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na
kulikuwa na ulinzi mkali wa kuzuia waandishi wa habari kufanya naye
mahojiano.
Hali ya Askofu Laizer
imekuwa tete, baada ya kuwapo kwa habari zisizo na uhakika kuwa amehamishiwa
katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mkoani Kilimanjaro.
Hata hivyo, jana ukweli
wa taarifa hizo ulibainika kuwa kiongozi huyo wa kiroho amelazwa katika
Hospitali ya Selian jijini hapa, baada ya Waziri Mkuu
kumtembelea.
NIPASHE lilijaribu
kuzungumza na watumishi wa hopsitali hiyo, ambao hawakutaka kutajwa majina yao
na kusema hali ya afya ya Askofu Laizer siyo nzuri na kwamba watu wanapaswa
kumwombea.
Lakini pia hawakuwa
tayari kutaja ugonjwa unaomsumbua Askofu huyo kwa kudai kuwa wao siyo
wasemaji.
Kabla ya Waziri Mkuu
Pinda kufika hospitalini hapo, asubuhi, alifungua mkutano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, unaoshughulikia masuala ya gesi na mafuta na baadaye mchana
alitembelea kituo cha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha SOS,
kilichopo Ngaramtoni, nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Akiwa katika kituo hicho
Waziri Mkuu Pinda alitoa Shilingi milioni 20 kuwasaidia watoto hao na kuwaomba
wadau wengine wenye uwezo kujitokeza kusaidia
watoto
Post a Comment