Wasira akisaini kitabu cha waombolezaji kwa niaba ya Rais
*********
RAIS Jakaya Kikwete
ametoa rambirambi kufuatia kifo cha muasisi wa TANU/CCM na mzalendo wa kwanza
kuwa mkuu wa Kanisa la KKKT- Dayosisi ya kati kutoka kwa wamisionari, mchungaji
Thomas Musa(86). Marehemu Thomas Musa aliyezaliwa desemba 6,1927 wilayani Iramba
alifariki ijumaa iliyopita na
kuzikwa jumanne wiki
hii, kijijini kwake Kinampanda, Iramba, mkoani Singida.
Katika salamu
zilizotolewa jana jumatano jioni nyumbani kwa marehemu na waziri wa nchi ofisi
ya Rais Stephen Wasira, Rais amesema amesikitishwa sana na kifo hicho kutokana
na mchango wa marehemu kwa taifa, hasa elimu na afya katika uhai
wake.
Rais alisema CCM na
Serikali yake inaungana na familia ya mjane na mtoto wa marehemu Jaji Kipenka
Musa anayesimamia familia hiyo, katika kipindi hiki kigumu cha
majonzi.
Katika rambirambi hiyo
ambayo hakutaka itangazwe, Rais amesema ingawa mzee Musa amefariki, lakini
matendo yake daima yataendelea kukumbukwa na kuenziwa kwa ajili ya maendeleo ya
taifa
Post a Comment