Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa mkoa wa Lindi waliohudhuria sharehe za kutimiza miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo kata ya Chiponda mkoani Lindi tarehe 5.2.2013.
Mke wa Rais na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Lindi
Mjini Mama Salma Kikwete akifungua rasmi jengo la CCM Tawi la Rondo kata ya
Chiponda huko Lindi Vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 36
ya CCM zilizofanyika kimkoa kijijii hapo tarehe 5.2.2013. Kulia kwa Mama Salma
ni Mjumbe wa NEC Taifa, Mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.
Mke wa Rais na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Lindi
Mjini Mama Salma Kikwete akifurahia mara baada ya kulifungua rasmi jengo la
CCM Tawi la Rondo kata ya Chiponda huko Lindi Vijijini wakati wa kilele cha
sherehe ya kutimiza miaka 36 ya CCM zilizofanyika kimkoa kijijii hapo tarehe
5.2.2013. Kulia kwa Mama Salma ni Mjumbe wa NEC Taifa, Mbunge wa Mtama na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard
Membe.
Ngoma ya Linyamwa ya kabila la
Wamwera ikichezwa na wananchi wa kijiji cha Mpenda kutoka wilaya ya Lindi
vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa Chama Cha
Mapinduzi zilizoazimishwa kimkoa katika kijiji cha Rondo tarehe
5.2.2013.
Mama Salma Kikwete aliyekuwa
mgeni rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 36 ya CCM Mkoani Lindi akijumuika
na wacheza ngoma ya Linyamwa kucheza ngoma hiyo. Sherehe hizo zilifanyika katika
kijiji cha Rondo huko Lindi vijijini tarehe 5.2.2013.
Mjumbe wa NEC na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe akimvisha
skafu Bwana Omary Issa kutoka Chama cha Wananchi, CUF, akiwa ni miongoni mwa
wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka vyama vingine vya siasa wakati wa
kilele cha sherehe za kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa chama
hicho.
Mjumbe wa NEC Taifa kutoka
wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya
ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja wakati wa sherehe za kutimiza
miaka 36 ya chama hicho zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo huko Lindi
Vijini tarehe 5.2.2013,
Post a Comment