Na Mroki Mroki, FK BLG
Kigoma
Makamu Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula amewasili mkoani Kigoma asubuhi
hii kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kupongeza mabadiliko
makubwa yaliyopo mkoani humo hasa Uwanja huo wa Ndege ambao unaonekana sasa kuwa
wa kisasa.
Mangula ambaye amepata
mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nappe
Nnauye pamoja na mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho ambaye ni Katibu wa Siasa
na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali
Mstaafu. Issa Machibya pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na
serikali.
Mangula amesema Kigoma ya
sasa si Kigoma aliyo ijua miaka iliyopita na viongozi wanastahili pongezi kwa
maendeleo hayo ya sekta mbalimbali.
“Kigoma ya leo sio Kigoma
ile ya zamani ..uwanja huu wakati ndege inataka kutua nilitaraji nitasikia
matairi ya kihangaika lakini nikashangaa tunakwenda vizuri tu” alisema Mangula
akishangiliwa na wakazi wa Kigoma.
Aidha amewaambia wakazi wa
Mkoa wa Kigoma kutembea kifua mbele kutoka na mafanikio makubwa yaliyofikiwa
hasa katika ujenzi wa uwanja wa ndenge wa kigoma ambao zamani haukuwa na tabaka
la lami ambapo sasa uwanja huo umewekewa tabaka la lami na kuondoa usumbufu
waliokuwa wakiupata zamani wananchi wa Kigoma.
Pia Mangula amewataka
wakazi wa mkoa huo kuendelea kupuuza kejeli zinazoendelea kutolewa na wanasiasa
wa upinzani kuwa mkoa wa kigoma umesahaurika kitu ambacho amesema hakina ukweli
kwani mkoa huo sasa umefunguka kwa miundombinu ya barabara.
Wakati huo huo, katika
kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ccm, mwenyekiti wa CCM
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho mkoani hapa kwa ajili ya
maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 3, 2013 katika
uwanja wa Michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea ambapo sasa yamefikia asilimia zaidi ya themnini na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pamoja na wajumbe wa NEC na viongozi wengine wa CCM wanataraji kwenda kukagua maandalizi hayo jioni ya leo.
Post a Comment