Wakazi wa Mtaa wa Kwa
Msisiri A na Bwanwani, Kata ya Mwanayamala, Manispaa ya Kinondoni wakishirikiana
na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, Diwani wa Kata hiyo, Songoro Mnyonge na
Mkuu wa Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana kufanya usafi katika Mtaa wa kwa Msisiri
A, Dar es Salaam mwishoni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kuweka mazingira
safi Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki.
Diwani wa Kata ya
Mwanayamala, Songoro Mnyonge akimpa maelezo Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph
Mwenda (wa tatu kulia) kuhusu mkakati wa kuboresha mtaro wa kupitisha majitaka
uliopo katika Mtaa wa Bwawani, wakati wa mwendelezo wa kampeni ya kuweka
mazingira safi Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkuu wa
Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Mtaa wa
Bwawani, Mohamed Mkandu (kulia).
Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph mwenda (wa pili kushoto) akikagua ujenzi holela wa moja ya
nyumba ya mkazi wa Mtaa wa Bwawani (kushoto), Kata ya Mwananyamala, Manispaa
hiyo unaopelekea kujaa kwa madimbwi ya maji wakati wa zoezi la kuhamasisha
uwekaji safi mazingira mwishoni mwa wiki ikiwa ni kampeni endelevu aliyoizindua
hivi karibuni. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata hiyo, Songoro Mnyonge na
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Mtaa wa Bwani, Mohamed Mkandu.
Wakazi wa Mtaa wa Kwa
Msisiri A na Bwawani, Kata ya Mwananyamala, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam
wakizibua moja ya chemba za mitaro ya kupitishia majitaka wakati wa zoezi la
uhamasishaji usafi wa mazingira lililoendeshwa na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph
Mwenda, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jordan Rugimbana na Diwani wa Kata hiyo, Songoro
Mnyonge.
Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akizungumza na viongozi na wakazi wa Kata ya
Mwananyamala, Manispaa hiyo wakati wa zoezi endelevu la uhamasishaji usafi wa
mazingira katika Kata hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Kata
hiyo.
Wakazi wa Mtaa wa Kwa
Msisiri A na Bwawani, Kata ya Mwananyamala, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam
wakishhudia kijiko cha Manispaa hiyo kikizibua moja ya chemba za mitaro ya
kupitishia majitaka wakati wa zoezi la uhamasishaji usafi wa mazingira
lililoendeshwa na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, Mkuu wa Wilaya hiyo,
Jordan Rugimbana na Diwani wa Kata hiyo, Songoro Mnyonge.
Post a Comment